Waefeso 3
3
Huduma ya Paulo kwa Mataifa
1 #
Flp 1:7,13; Kol 1:24 Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; 2#Kol 1:25 ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; 3#Efe 1:9,10; Kol 1:26 ya kwamba kwa kufunuliwa nilijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. 4#Kol 1:26-27 Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. 5Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii nyakati hizi katika Roho; 6#Efe 2:13,18,19 ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; 7#Kol 1:25,29 Injili hiyo ambayo nilifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. 8#1 Kor 15:9,10; Efe 1:7; Gal 1:16 Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; 9#Rum 16:25; Kol 1:26,27 na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; 10#1 Pet 1:12; Rum 11:33; Kol 1:26 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; 11#Efe 1:11 kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu. 12#Yn 14:6; Ebr 4:16; Rum 5:2 Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini. 13#Kol 1:24 Basi naomba msikate tamaa kwa sababu ya dhiki zangu kwa ajili yenu, zilizo utukufu wenu.
Ombi kwa wasomaji
14Kwa hiyo nampigia Baba magoti, 15ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, 16#Efe 1:7; 6:10; Kol 1:11 awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. 17#Yn 14:23; Kol 1:23; 2:7 Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; 18#Kol 2:2 ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; 19#Kol 2:3 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
20 #
Kol 1:29
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; 21naam, atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.
Currently Selected:
Waefeso 3: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: