Waefeso 6
6
Watoto na wazazi
1 #
Kol 3:20
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2#Kut 20:12; Kum 5:16 Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia. 4#Kol 3:21; Isa 50:5; Mit 2:2; 3:11; 19:18; Kum 6:7,20-25; Zab 78:4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Watumwa na mabwana
5 #
Kol 3:22-25; Tit 2:9,10; 1 Pet 2:18 Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba mnamtii Kristo; 6wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; 7kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu; 8#2 Kor 5:10 mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana awe ni mtumwa au ni mtu huru. 9#Kum 10:17; Kol 3:25; 4:1; 2 Nya 19:7; Mdo 10:34 Nanyi, mabwana, watendeeni wao yayo hayo, pasipo kuwatisha, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.
Silaha zote za Mungu
10 #
1 Kor 16:13; 1 Yoh 2:14 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11#Efe 4:14; 2 Kor 10:4 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12#Efe 2:2; Yn 14:30; Kol 1:13; 1 Pet 5:8,9 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13#1 Fal 20:11 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14#Isa 11:5; 59:17; Lk 12:35; 1 Pet 1:13; 1 The 5:8 Basi simameni, mkiwa mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15#Isa 52:7; 40:3,9 na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani; 16#1 Pet 5:9; 1 Yoh 5:4 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17#Isa 59:17; 11:4; 49:2; 51:16; 1 The 5:8; Hos 6:5 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18#Mt 26:41; Kol 4:2,3 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; 19#Kol 4:3; 2 The 3:1; Mdo 4:29 pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili; 20#2 Kor 5:20; Kol 4:4 ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.
Mambo ya binafsi na baraka
21 #
Mdo 20:4; 2 Tim 4:12; Kol 4:7 Basi ili nanyi pia mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote; #Kol 4:7-8 22#Kol 4:7,8 ambaye ninamtuma kwenu kwa kusudi lilo hilo mpate kuzijua habari zetu, naye awafariji mioyo yenu.
23Amani na iwe kwa ndugu, na upendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo. 24#1 Pet 1:8 Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo usioisha.
Currently Selected:
Waefeso 6: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: