Ezekieli 41
41
1 #
Zek 6:12; Mt 16:18; 1 Kor 3:16; 2 Kor 6:16; Efe 2:21; Ufu 3:12 Akanileta mpaka hekaluni, akaipima miimo, upana wake dhiraa sita upande mmoja, na upana wake dhiraa sita upande wa pili, ambao ulikuwa ni upana wa maskani. 2Na upana wa maingilio yake ulikuwa dhiraa kumi; na mbavu za maingilio zilikuwa dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; akaupima urefu wake, dhiraa arubaini, na upana wake, dhiraa ishirini. 3Kisha akaingia ndani, akapima kila mwimo wa maingilio, dhiraa mbili; nayo maingilio, dhiraa sita; na upana wa maingilio dhiraa saba. 4#1 Fal 6:20; 2 Nya 3:8; Ufu 21:2,3,16,17 Akaupima urefu wake; dhiraa ishirini, na upana wake, dhiraa ishirini, mbele ya hekalu; akaniambia, Hapa ndipo mahali patakatifu kuliko kila mahali. 5Kisha akaupima ukuta wa nyumba, dhiraa sita; na upana wa kila chumba cha mbavuni, dhiraa nne, kuizunguka nyumba pande zote. 6#1 Fal 6:5,6 Na vile vyumba vya mbavuni vilikuwa na ghorofa tatu, moja juu ya mwenziwe; vilikuwa thelathini, safu baada ya safu; navyo viliingia ndani ya ukuta uliokuwa wa nyumba, kwa vile vyumba vya mbavuni pande zote vipate kushikamana nao, wala visishikamane na ukuta wa nyumba. 7Na vile vyumba vya mbavuni vilizidi kuwa vipana, kwa kadiri vilivyoizunguka nyumba juu kwa juu; maana kule kuzunguka kwake kulikwenda juu kwa juu, kuizunguka nyumba; basi upana wa nyumba ulikuwa ule ule hadi juu; basi hupanda juu toka chumba cha chini hadi chumba cha juu, kwa njia ya kile chumba cha katikati. 8#Isa 28:16; Eze 40:5 Tena, nikaona ya kwamba nyumba ile ilikuwa na sakafu ya mawe, iliyoinuliwa pande zote; nayo misingi ya vyumba vya mbavuni ilikuwa mwanzi mzima wa dhiraa sita. 9Unene wa ukuta uliokuwa wa vile vyumba vya mbavuni, upande wa nje, ulikuwa dhiraa tano; nayo nafasi iliyobaki ilikuwa dhiraa tano; na kati ya vyumba vya mbavuni vya nyumba, 10na vyumba vya walinzi, upana wa dhiraa ishirini, kuizunguka nyumba pande zote. 11Na milango ya vile vyumba vya mbavuni iliielekea nafasi ile iliyobaki, mlango mmoja ulielekea upande wa kaskazini, na mlango mmoja upande wa kusini; na upana wa nafasi iliyobaki ulikuwa dhiraa tano pande zote. 12Nalo jengo lililokabili mahali palipotengeka upande wa magharibi, upana wake dhiraa sabini; na ukuta wa lile jengo, unene wake dhiraa tano pande zote, na urefu wake dhiraa tisini. 13Basi akaipima nyumba, urefu wake dhiraa mia moja; na mahali pale palipotengeka na jengo lile, pamoja na kuta zake, urefu wake dhiraa mia moja; 14tena upana wa uso wa nyumba, na wa mahali palipotengeka upande wa mashariki, dhiraa mia.
15Akaupima urefu wa jengo lile lililokabili mahali palipotengeka, palipokuwa nyuma yake, na baraza zake upande huu na upande huu, dhiraa mia moja; na hekalu la ndani, na kumbi za ua; 16#1 Fal 7:4; Isa 54:12; Eze 40:16; 1 Kor 13:12 na vizingiti, na madirisha yaliyofungwa, na baraza za pande zote za ghorofa zile tatu, zilizokikabili kizingiti, zilitiwa mabamba ya mti pande zote; na toka chini hadi madirishani; (nayo madirisha yamefunikwa); 17na mpaka juu ya mlango hata nyumba ya ndani, na nje, na juu ya kuta zote pande zote, katika nyumba ya ndani, na ya nje, 18#Mwa 3:24; Kut 25:22; 1 Sam 4:4; 2 Sam 22:11; 1 Fal 6:29; 2 Nya 3:10; Zab 80:1; 99:1; Eze 10:2,14; 1:10; Ufu 4:7-9 kulipambwa kwa makerubi na mitende; mtende mmoja kati ya kerubi na kerubi, na kila kerubi lilikuwa na nyuso mbili; 19basi palikuwa na uso wa mwanadamu kuelekea mtende mmoja, na uso wa mwanasimba kuelekea mtende wa pili; ndivyo vilivyofanyika katika nyumba nzima pande zote. 20Toka chini hadi juu ya mlango makerubi yamefanyika, na mitende, na vivi hivi ukuta wa hekalu. 21Na hilo hekalu, miimo ya milango yake ilikuwa ya miraba; na mbele ya patakatifu kuonekana kwake palionekana kama hapo kwanza. 22#Kut 30:1,8; 1 Fal 7:48; 2 Nya 4:19; Ufu 8:3; Mit 9:2; Wim 1:12; Eze 44:16; Mal 1:7,12 Madhabahu ilikuwa ni ya miti, kimo chake dhiraa tatu, na urefu wake dhiraa mbili; na pembe zake, na msingi wake, na kuta zake zilikuwa za miti; akaniambia, Hii ndiyo meza iliyo mbele za BWANA. 23#1 Fal 6:31-35 Nalo hekalu na patakatifu palikuwa na milango miwili. 24Na milango hiyo, kila mmoja ulikuwa na mbao mbili; mbao mbili zigeukazo; mbao mbili za mlango mmoja, na mbao mbili za mlango wa pili. 25Na milango ya hekalu ilitengenezwa makerubi na mitende vile vile, kama zile kuta zilivyotengenezwa; tena palikuwa na boriti nene juu ya uso wa ukumbi, nje. 26#Eze 40:16 Tena palikuwa na madirisha yaliyofungwa, na mitende, upande huu na upande huu, katika pande za ukumbi; ndiyo habari ya vyumba vya mbavuni vya nyumba hiyo, na vya boriti zile nene.
Currently Selected:
Ezekieli 41: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: