YouVersion Logo
Search Icon

Ezekieli 48

48
Mgawanyo wa nchi
1 # Hes 34:7-9; Eze 47:15 Basi, haya ndiyo majina ya makabila hayo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hadi maingilio ya Hamathi, hadi Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja. 2Tena mpakani mwake Dani, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Asheri, fungu moja. 3Na mpakani mwa Asheri, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Naftali, fungu moja. 4Na mpakani mwa Naftali, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Manase, fungu moja. 5Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja. 6Na mpakani mwa Efraimu, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Reubeni, fungu moja. 7Na mpakani mwa Reubeni, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Yuda, fungu moja.
8 # Eze 45:1 Na mpakani mwa Yuda, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi, yatakuwapo matoleo mtakayotoa, upana wake mianzi elfu ishirini na tano, na urefu wake sawasawa na moja la mafungu hayo, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; na mahali patakatifu ni katikati yake. 9Matoleo hayo, mtakayomtolea BWANA, urefu wake ni mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake elfu kumi. 10Maeneo hayo matakatifu yatakuwa kwa ajili ya makuhani; upande wa kaskazini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano, na upande wa magharibi upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa mashariki upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa kusini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano; na mahali patakatifu pa BWANA patakuwa katikati yake. 11#2 Nya 29:4,5; Neh 9:34; Yer 23:11; Eze 22:26; 44:10; Sef 3:4; Mal 2:7,8 Patakuwa kwa makuhani wa wana wa Sadoki, waliotakasika, waliofuata maagizo yangu, wasioasi, wana wa Israeli walipoasi, kama Walawi walivyoasi. 12Na matoleo hayo ya nchi yatolewayo, yatakuwa kwao kitu kitakatifu sana, karibu na mpaka wa Walawi. 13Na kuukabili mpaka wa makuhani, Walawi watakuwa na fungu, urefu wake mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake mianzi elfu kumi; urefu wote utakuwa mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake mianzi elfu kumi. 14#Kut 22:29; Law 27:10 Wala hawatauza sehemu yake, wala kuibadili, wala hawatawapa wengine malimbuko ya nchi; maana ni matakatifu kwa BWANA. 15#Kum 20:5; Eze 42:20; 44:23; 45:6 Na mianzi elfu tano iliyosalia katika upana, kuikabili hiyo elfu ishirini na tano, itatumiwa na watu wote, kwa huo mji, na kwa maskani, na kwa viunga, na huo mji utakuwa katikati yake. 16Na vipimo vyake ni hivi; upande wa kaskazini mianzi elfu nne na mia tano, na upande wa kusini mianzi elfu nne na mia tano, na upande wa mashariki mianzi elfu nne na mia tano, na upande wa magharibi mianzi elfu nne na mia tano. 17Nao mji utakuwa na malisho; upande wa kaskazini mianzi mia mbili na hamsini, na upande wa kusini mianzi mia mbili na hamsini, na upande wa mashariki mianzi mia mbili na hamsini, na upande wa magharibi mianzi mia mbili na hamsini. 18Na mabaki ya urefu wake yaelekeayo matoleo matakatifu, upande wa mashariki yatakuwa mianzi elfu kumi, na upande wa magharibi mianzi elfu kumi; nayo yatakuwa sawasawa na matoleo matakatifu; na mazao yake yatakuwa ni chakula cha watu wafanyao kazi humo mjini. 19#Ufu 7:5 Na hao wafanyao kazi mjini, wa kabila zote za Israeli, watailima nchi hiyo. 20#Hes 24:5; Isa 33:20; Ufu 21:16 Matoleo yote yatakuwa mianzi elfu ishirini na tano, kwa mianzi elfu ishirini na tano; mtatoa matoleo matakatifu, nchi ya mraba, pamoja na milki ya mji.
21 # Yos 18:1; Isa 2:2; 11:10; Hos 1:11; Hag 2:7,9; Mt 11:28; 13:16,17; Yn 12:32; Rum 15:9,12; Ufu 2:1; 21:3 Nayo mabaki yake yatakuwa ya huyo mkuu, upande huu na upande huu wa matoleo matakatifu, na milki ya mji, kuikabili hiyo mianzi elfu ishirini na tano ya matoleo, kuelekea mpaka wa mashariki; tena upande wa magharibi kuikabili hiyo mianzi elfu ishirini na tano, upande wa kuelekea mpaka wa magharibi; sawa na yale mafungu, hayo yatakuwa ya huyo mkuu; na matoleo matakatifu na mahali patakatifu pa nyumba patakuwa katikati yake. 22Tena tokea milki ya Walawi, na tokea milki ya mji, kwa kuwa ni katikati ya nchi iliyo ya mkuu, katikati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini, itakuwa ya mkuu.
23Na katika habari za kabila zilizosalia; toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Benyamini, fungu moja. 24Tena mpakani mwa Benyamini, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Simeoni, fungu moja. 25Tena mpakani mwa Simeoni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Isakari, fungu moja. 26Na mpakani mwa Isakari, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Zabuloni, fungu moja. 27Na mpakani mwa Zabuloni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Gadi, fungu moja. 28#2 Nya 20:2; Eze 47:19; Mwa 15:18; Hes 34:15; Yos 15:47; Isa 27:12 Na mpakani mwa Gadi, upande wa kusini kuelekea kusini, mpaka wake utakuwa toka Tamari, mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa. 29#Eze 47:14,21,22 Hiyo ndiyo nchi mtakayoyagawanyia makabila ya Israeli, kuwa urithi wao, na hayo ndiyo mafungu yao, asema Bwana MUNGU.
30 # Ufu 21:12-13 Na matokeo ya mji ndiyo haya; upande wa kaskazini, mianzi elfu nne na mia tano, kwa kipimo; 31#Isa 60:18; Ufu 21:12 na malango ya mji yatatajwa kwa majina ya makabila ya Israeli, malango matatu upande wa kaskazini; lango la Reubeni, moja; lango la Yuda, moja; na lango la Lawi, moja. 32Na upande wa mashariki, mianzi elfu nne na mia tano, kwa kipimo; na malango matatu; lango la Yusufu, lango la Benyamini; lango la Dani. 33Na upande wa kusini, mianzi elfu nne na mia tano kwa kupima; na malango matatu; lango la Simeoni; lango la Isakari, lango la Zabuloni. 34Na upande wa magharibi, mianzi elfu nne na mia tano; pamoja na malango yake matatu; lango la Gadi, lango la Asheri; na lango la Naftali. 35#Zab 72:8; Isa 2:2; Mal 1:11; Kut 17:15; Amu 6:24; Ufu 21:3 Kuuzunguka ni mianzi elfu kumi na nane; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo.

Currently Selected:

Ezekieli 48: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in