Mwanzo 32
32
1 #
Zab 91:11; Ebr 1:14 Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye. 2#Yos 5:14; 2 Fal 6:16; Zab 103:21; 148:2; Lk 2:13 Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu.
Yakobo amtumia Esau zawadi
3 #
Mwa 33:14; 36:6-8; Kum 2:5; Yos 24:4 Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu. 4#Mit 15:1 Akawaagiza akisema, Mwambieni hivi bwana wangu, Esau, Hivi ndivyo asemavyo mtumwa wako, Yakobo; Nimekaa ugenini kwa Labani, na kukawia huko hata sasa, 5#Mwa 30:43; 33:8 nami nina ng'ombe, na punda, na kondoo, na watumwa, na vijakazi; nami nimepeleka watu nimpashe bwana wangu habari, nipate neema machoni pako.
6 #
Mwa 33:1
Wale wajumbe wakarudi kwa Yakobo wakisema, Tulifika kwa ndugu yako, Esau, naye anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye.
7 #
Mwa 35:3; Mit 2:11; Efe 5:15 Ndipo Yakobo akaogopa sana, na kufadhaika sana, akawagawanya watu waliokuwa pamoja naye, na kondoo, na ng'ombe, na ngamia, wawe makundi mawili. 8Akasema, Akija Esau kwa kundi la kwanza, akalipiga, kundi litakalosalia litaokoka.
9 #
Zab 50:15; Mwa 28:13; 31:3 Yakobo akasema, Ee Mungu wa baba yangu Abrahamu, na Mungu wa baba yangu Isaka, BWANA, uliyeniambia, Rudi uende mpaka nchi yako, na kwa jamaa zako, nami nitakutendea mema; 10#2 Sam 9:8; Mwa 24:27; Ayu 8:7 mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili. 11#Zab 59:1,2; Hos 10:14 Uniokoe sasa kutoka kwa mkono wa ndugu yangu, mkono wa Esau, maana mimi ninamwogopa, asije akaniua, na kina mama pamoja na watoto. 12#Mwa 22:17; Mwa 28:13-15 Nawe ulisema, Hakika nitakutendea mema, nami nitafanya uzao wako uwe kama mchanga wa bahari, usiohesabika kwa kuwa mwingi.
13 #
Mwa 43:11
Akakaa huko usiku ule. Kisha akatwaa baadhi ya vitu alivyokuwa navyo, kuwa zawadi kwa Esau, nduguye; 14mbuzi majike mia mbili, mbuzi dume ishirini, kondoo majike mia mbili, na kondoo dume ishirini; 15ngamia wanyonyeshao thelathini pamoja na wana wao, ng'ombe majike arubaini na mafahali kumi; punda wake ishirini na wana wao kumi. 16Akawatia mkononi mwa watumwa wake, kila kundi peke yake. Naye akawaambia watumwa wake, Vukeni mbele yangu, mkaache nafasi kati ya kundi na kundi. 17Akamwagiza yule wa kwanza akasema, Esau, ndugu yangu, akikukuta, na kukuuliza, akisema, Wewe ni wa nani? Unakwenda wapi? Tena ni wa nani hawa walio mbele yako? 18Basi, useme, Ni wa mtumwa wako, Yakobo, ni zawadi, aliyompelekea bwana wangu, Esau. Na tazama, yeye mwenyewe yuko nyuma yetu.
19Akamwagiza tena wa pili, na wa tatu, wote waliofuata makundi, akisema, Hivi ndivyo mtakavyomwambia Esau, akiwakuta. 20#Mit 21:14 Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu. 21Basi ile zawadi ikavuka mbele yake, naye mwenyewe akakaa usiku ule kambini.
Yakobo apambana na Penieli
22 #
Kum 3:16
Akaondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. 23Akawatwaa, akawavusha mto, akavusha na vyote alivyokuwa navyo.
24 #
Hos 12:3-4
Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. 25#Mt 26:41; 2 Kor 12:7 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. 26#Lk 24:28; Hos 12:4; 2 Fal 17:34 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki. 27Akamwuliza, Jina lako ni nani? Akasema, Yakobo. 28#Mwa 35:10; Hos 12:3,4; Mwa 25:31; 27:33 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda. 29#Amu 13:17-18 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko. 30#Mwa 16:13; Kut 24:11; 33:20; Kum 5:24; Amu 6:22; 13:22; Isa 6:5 Yakobo akapaita mahali pale, Penieli,#32:30 Penieli: Katika Kiebrania ni ‘uso wa Mungu’. maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.
31Jua likamzukia akivuka Penueli, akachechemea kwa sababu ya paja la mguu wake. 32Kwa hiyo wana wa Israeli hawali ule mshipa ulio katika uvungu wa paja hata leo; maana alimgusa Yakobo panapo uvungu wa paja katika mshipa wa kiuno.
Currently Selected:
Mwanzo 32: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: