Waraka kwa Waebrania 2
2
Onyo kuhusu kuwa makini
1Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo tuliyoyasikia tusije tukayakosa. 2#Mdo 7:38,53; Gal 3:19 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, 3#Ebr 10:29; 12:25 sisi je! Tutapataje kupona, tukipuuza wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliomsikia; 4#Mk 16:20; 1 Kor 12:4,11 Mungu naye akishuhudia pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
Kutukuka kwa kujishusha
5Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema,
6 #
Zab 8:4-6
Mwanadamu ni nini hata umkumbuke,
Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?
7Umemfanya mdogo kwa muda kuliko malaika,
Umemvika taji la utukufu na heshima,
Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
8 #
1 Kor 15:27
Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake.
Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakubakiza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hamjaona vitu vyote kutiwa chini yake, 9#Flp 2:8,9 ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo kwa muda kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji la utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu. 10#Rum 11:36 Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. 11#Mk 3:34,35; Mt 25:40; Yn 20:17 Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake; 12#Zab 22:22 akisema,
Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu;
Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.
13 #
Isa 8:17,18; 2 Sam 22:3 Na tena,
Nitakuwa nimemtumaini yeye.
Na tena,
Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.
14 #
2 Tim 1:10; Yn 12:31; Ufu 12:10; 1 Kor 15:56 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 15awaache huru wale ambao katika maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 16#Isa 41:8,9 Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Abrahamu. 17#Zab 22:22; Flp 2:7 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye kafara ya suluhu kwa dhambi za watu wake. 18#Ebr 4:15 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Currently Selected:
Waraka kwa Waebrania 2: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: