Waraka kwa Waebrania UTANGULIZI
UTANGULIZI
Waraka huu hautaji jina la mwandishi, walengwa wake wala mahali ulikotumwa. Hata hivyo, kutokana uandishi wake, inaonekena kwamba mwandishi huyo aliwaandikia Wakristo walioongoka kutoka dini ya Kiyahudi na ambao imani yao ilikuwa inafifia. Anawatia moyo wasikate tamaa kwa kuwa Kristo ametimiza yote yaliyotakiwa katika Agano la Mungu.
Kwa namna ya pekee kabisa Mwandishi anazingatia kuonesha hali ya pekee ya Yesu, Mwana wa Mungu: yeye ni mkuu kuliko vitu vyote (1:2-4), Mkuu juu ya malaika (1:4—2:18), Mkuu kuliko Musa (3:1—4:13) au ukuhani wa Walawi (4:14—7:28). Yesu ni Kuhani Mkuu ambaye alipenyeza mpaka mbinguni (4:14) na ambaye kwa damu yake alitufungulia njia mpya na hai “tupate kuingia katika mahali patakatifu mno” (10:19-20). Wakati Torati ya Musa na ibada za Agano la Kale zilipofanyika mara nyingi pamoja na taratibu zake za sadaka nyingi na ibada zilizokuwa ngumu sana kuelewa, Kristo alichukua mwili wake mwenyewe kama sadaka iliyofanyika “mara moja tu milele” (9:26-28; 10:10,14), akawa mdhamini (7:22) wa Agano Jipya la daima.
Baada ya kueleza ukuu wake Yesu Kristo, katika sura 10:19—13:17 Mwandishi anawahimiza walengwa wake wadumu imara kwa kuwapa, baadhi ya mengineyo, mifano kutoka Agano la Kale ya watu waliodumu katika imani.
Currently Selected:
Waraka kwa Waebrania UTANGULIZI: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: