YouVersion Logo
Search Icon

Hosea 2

2
1Waambieni ndugu zenu, Ami#2:1 Ami: maana yake ni ‘watu wangu.’ na dada zenu, Ruhama.#2:1 Ruhama: maana yake ni ‘aliyehurumiwa.’
Uzinzi, adhabu na ukombozi wa Israeli
2 # Isa 50:1; Yer 3:1,9,13; Eze 16:25; Hos 1:2 Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na aondokane na usherati wake usiwe mbele ya uso wake, na uzinzi wake usiwe kati ya matiti yake; 3#Yer 13:22; Eze 19:13; Amo 8:11 nisije nikamvua nguo zake akawa uchi, nikamweka katika hali aliyokuwa nayo siku ya kuzaliwa kwake, na kumfanya kama jangwa, na kumweka kama nchi kame, na kumwua kwa kiu; 4naam, sitawaonea rehema watoto wake; kwa maana ni watoto wa uzinzi. 5#Yer 44:17 Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu. 6#Ayu 19:8 Basi kwa ajili ya hayo, angalia, nitaiziba njia yako kwa miiba, nami nitafanya kitalu juu yake, asipate kuyaona mapito yake. 7#Lk 15:18; Eze 16:8 Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa. 8Maana hakujua ya kuwa mimi ndiye niliyempa ngano, na divai, na mafuta, na kumwongezea fedha na dhahabu, walivyovitumia kwa ajili ya Baali. 9Basi kwa ajili ya hayo, nitaitwaa tena ngano yangu kwa wakati wake, na divai yangu kwa wakati wake, nami nitamnyang'anya sufu yangu na kitani yangu, vya kumfunika uchi wake. 10Na sasa nitaifunua aibu yake mbele ya macho ya wapenzi wake, wala hapana mtu atakayemwokoa katika mkono wangu. 11#Isa 24:7; Yer 7:34; Amo 8:10 Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa. 12#Isa 5:5 Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila. 13#Amu 3:7; Eze 23:40 Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA.
14 # Eze 20:35 Kwa hiyo angalia, mimi nitamshawishi, na kumleta nyikani, na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo. 15#Isa 65:10; Omb 3:21; Zek 9:12; 1 Kor 13:13; Yos 7:24-26 Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri. 16Tena siku hiyo itakuwa, asema BWANA, utaniita Ishi,#2:16 Ishi: maana yake ni Mume wangu. wala hutaniita tena Baali.#2:16 Baali: maana yake ni Bwana wangu. 17#Kut 23:13 Kwa maana nitayaondoa majina ya Mabaali kinywani mwake, wala hawatatajwa tena kwa majina yao. 18#Ayu 5:23; Zek 9:10; Isa 11:6; 2:4; Law 26:5; Yer 23:6 Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi; nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nitawalalisha salama salimini. 19Nami nitakuposa uwe wangu wa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema. 20#Isa 54:13; Yer 31:33 Nami nitakuposa kwa uaminifu; nawe utamjua BWANA. 21#Zek 8:12 Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema BWANA; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi; 22nayo nchi itaiitikia nafaka na divai na mafuta; nayo yataiitikia Yezreeli. 23#Zek 10:9; 13:9; Rum 9:25; 1 Pet 2:10 Nami nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu.

Currently Selected:

Hosea 2: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in