YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 32

32
Ufalme wenye haki watabiriwa
1 # 2 Nya 31:20; Zab 7:1,2; Yer 23:5; Zek 9:9; Ebr 1:8,9; Ufu 19:11 Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu. 2Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu. 3#Isa 29:18 Tena macho yao waonao hayatakuwa na kiwi, na masikio yao wasikiao yatasikiliza. 4Tena moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu maarifa, na ndimi zao wenye kigugumizi zitakuwa tayari kunena sawasawa. 5Mpumbavu hataitwa tena muungwana, wala mlaghai hataitwa kuwa ni mheshimiwa. 6Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya BWANA, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa bila chakula, na kuwanyima kinywaji wenye kiu. 7Tena vyombo vyake mlaghai ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki. 8Bali muungwana huwaza mambo ya kiungwana, naye hushika sana mambo ya kiungwana.
Wanawake wasiojali waonywa juu ya maafa
9 # Amo 6:1 Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, isikieni sauti yangu; enyi binti za watu msiojali, tegeni masikio yenu msikie maneno yangu. 10Maana mtataabishwa kwa zaidi kidogo ya mwaka, enyi wanawake mliojikinai; kwa sababu mavuno ya mizabibu yatakoma, wakati wa kuvuna vitu vya mashamba hautakuja. 11Tetemekeni, enyi wanawake mnaostarehe; taabikeni, enyi msiokuwa na uangalifu; jivueni, jivueni nguo zenu kabisa, na kujivika nguo za magunia viunoni. 12Watajipiga vifua kwa ajili ya mashamba mazuri, kwa ajili ya mzabibu uliozaa sana. 13#Hos 9:6 Juu ya nchi ya watu wangu itamea michongoma na mibigili; naam, juu ya nyumba za furaha katika mji ulio na shangwe; 14maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda mwitu, malisho ya makundi ya kondoo; 15#Zab 104:30 hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.
Amani ya utawala wa Mungu
16 # Zek 8:3 Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana. 17#Zab 72:2,3; Mik 4:4,5; Lk 2:14 Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. 18Na watu wangu watakaa katika makao ya amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu. 19#Zek 11:2 Lakini mvua ya mawe itanyesha, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika. 20#Isa 30:24 Heri ninyi mpandao mbegu kando ya maji yote, na kuiacha miguu ya ng'ombe na punda waende kokote.

Currently Selected:

Isaya 32: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in