Ayubu 14
14
1 #
Ayu 15:14; Zab 51:5; Mhu 2:23 Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke
Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
2 #
Isa 40:6; Yak 1:10; 1 Pet 1:24 Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa;
Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.
3 #
Zab 144:3; 143:2 Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye,
Na kunitia katika hukumu pamoja nawe?
4 #
Mwa 5:3; Zab 51:5; Yn 3:5; Rum 5:12; Efe 2:3 Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye.
5Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe,
Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;
6 #
Zab 39:13
Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika,
Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.
7Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena,
Wala machipukizi yake hayatakoma.
8Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani,
Na shina lake kufa katika udongo;
9Lakini kwa harufu ya maji utachipuka,
Na kutoa matawi kama mche.
10Lakini mwanadamu hufa, hufariki dunia;
Naam, mwanadamu hukata roho, naye yupo wapi?
11Kama vile maji kupwa katika bahari,
Na mto kupunguka na kukatika;
12 #
Zab 102:26; Isa 51:6; Mdo 3:21; Rum 8:20; 2 Pet 3:7; Ufu 20:14 Ndivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke;
Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka,
Wala kuamshwa usingizini.
13Laiti ungenificha kuzimuni,
Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita,
Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!
14 #
Ayu 13:15; Zab 16:10; 1 Kor 15:42-58; Flp 3:21 Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena?
Mimi ningengoja siku zote za huduma yangu,
Hadi kufunguliwa kwangu kunifikie.
15 #
Ayu 13:22; Zab 50:4; Yn 5:28; 1 The 4:16 Wewe ungeita, nami ningekujibu;
Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako.
16 #
Kum 32:34; Ayu 10:6,14; 13:27; Zab 56:8; Mit 5:21; Yer 32:19; Hos 13:12 Lakini sasa wazihesabu hatua zangu;
Je! Huchungulii dhambi yangu?
17Kosa langu limetiwa mhuri mfukoni,
Nawe waufunga uovu wangu.
18Lakini, tazama, mlima ukianguka hutoweka,
Nalo jabali huondolewa mahali pake;
19Maji mengi huyapunguza mawe;
Mafuriko yake huuchukua mchanga wa nchi;
Nawe matumaini ya wanadamu wayaangamiza.
20Wewe wamshinda nguvu sikuzote, naye hupita aende zake
Wabadili sura zake, na kumtuma aende mbali.
21 #
1 Sam 4:20; Zab 39:6; Mhu 9:5; Isa 63:16 Wanawe hufikia heshima, wala yeye hajui;
Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.
22 #
Zab 49:14; Mit 14:32; Mt 8:12 Huhisi tu maumivu ya mwili wake,
Na huombolezea nafsi yake tu.
Currently Selected:
Ayubu 14: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: