YouVersion Logo
Search Icon

Ayubu 4

4
Elifazi anena: Ayubu ametenda dhambi
1Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema,
2Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya?
Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene?
3Tazama, wewe umewafunza watu wengi,
Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge.
4Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka,
Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.
5 # Mit 24:10; Lk 4:23 Lakini sasa haya yamekufikia wewe, nawe wafa moyo;
Yamekugusa, nawe wafadhaika.
6 # Ayu 1:1; Mit 3:26 Je! Dini yako siyo tegemeo lako?
Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?
7Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia?
Au ni wapi hao waelekevu walikatiliwa mbali?
8 # Zab 7:14 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu,
Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.
9Kwa pumzi za Mungu huangamia.
Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.
10 # Ayu 29:17; Zab 3:7 Kunguruma kwake simba, na sauti ya simba mkali,
Na meno ya simba wachanga, yamevunjika.
11 # Zab 34:10 Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo,
Nao watoto wa simba jike wametawanyika mbalimbali.
12Basi, nililetewa neno kwa siri,
Sikio langu likasikia manong'ono yake.
13 # Ayu 33:15 Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku,
Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.
14Hofu iliniangukia na kutetemeka,
Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.
15 # Zab 104:4; Mt 14:26; Ebr 1:14 Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu;
Na nywele za mwili wangu zilisimama.
16Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake,
Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu;
Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,
17Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu?
Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?
18 # 2 Pet 2:4 Tazama, yeye hawategemei watumishi wake;
Na malaika wake huwahesabia kosa;
19Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo,
Ambazo misingi yao i katika mchanga,
Hao wanaopondwa kama nondo!
20Kati ya asubuhi na jioni huvunjwa-vunjwa;
Waangamia milele wala hapana atiaye moyoni.
21Je! Kamba ya hema yao haikung'olewa ndani yao?
Nao hufa hata bila kuwa na hekima.

Currently Selected:

Ayubu 4: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in