Maombolezo 3
3
Upendo wa Mungu huvumilia
1Mimi ni mtu aliyeona mateso
Kwa fimbo ya ghadhabu yake.
2Ameniongoza na kunipeleka katika giza
Wala si katika nuru.
3Hakika juu yangu augeuza mkono wake
Mara kwa mara mchana wote.
4Amechakaza ngozi yangu na nyama yangu;
Ameivunja mifupa yangu.
5Amejenga boma juu yangu,
Na kunizungusha uchungu na uchovu.
6 #
Zab 88:5
Amenikalisha penye giza,
Kama watu waliokufa zamani.
7Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka;
Amenifunga kwa mnyororo mzito.
8 #
Ayu 30:20; Zab 22:2 Naam, nikilia na kuomba msaada,
Huyapinga maombi yangu.
9Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa;
Ameyapotosha mapito yangu.
10 #
Hos 5:14
Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye,
Kama simba aliye mafichoni.
11 #
Hos 6:1
Amezigeuza njia zangu, na kuniraruararua;
Amenifanya ukiwa.
12 #
Ayu 6:4; Zab 34:2 Ameupinda upinde wake,
Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale.
13Amenichoma viuno
Kwa mishale ya podo lake.
14 #
Neh 4:2-4; Zab 22:6,7; Yer 20:7; Mt 27:29-31 Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote;
Wimbo wao mchana kutwa.
15 #
Yer 9:15
Amenijaza uchungu,
Amenikinaisha kwa pakanga.
16 #
Mit 20:17
Amenivunja meno kwa changarawe;
Amenifunika majivu.
17Umeniweka nafsi yangu mbali na amani;
Nikasahau kufanikiwa.
18 #
Zab 31:22
Nikasema, Nguvu zangu zimepotea,
Na tumaini langu kwa BWANA.
19Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu,
Pakanga na nyongo.
20Nafsi yangu ingali ikiyakumbuka hayo,
Nayo imeinama ndani yangu.
21Najikumbusha neno hili,
Kwa hiyo nina matumaini.
22 #
Neh 9:31; Zab 57:10; Mal 3:6 Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,
Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
23 #
Isa 33:2; Ebr 10:23 Ni mpya kila siku asubuhi;
Uaminifu wako ni mkuu.
24 #
Zab 16:5
BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu,
Kwa hiyo nitamtumaini yeye.
25 #
Zab 130:6
BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,
Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
26 #
Zab 37:7
Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA
Na kumngojea kwa utulivu.
27 #
Zab 90:12
Ni vema mwanadamu aichukue nira
Wakati wa ujana wake.
28 #
Yer 15:17
Na akae peke yake na kunyamaza kimya;
Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake.
29 #
Ayu 42:6
Na atie kinywa chake mavumbini;
Ikiwa yamkini liko tumaini.
30 #
Mik 5:1; Mt 5:39 Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake;
Ashibishwe mashutumu.
31 #
Zab 94:14
Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu
Hata milele.
32Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,
Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
33 #
Ebr 12:10
Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.
Wala kuwahuzunisha.
34Wafungwa wote wa duniani
Kupondwa chini kwa miguu,
35Kuipotosha hukumu ya mtu
Mbele zake Aliye Juu,
36 #
Hab 1:13
Na kumnyima mtu haki yake,
Hayo Bwana hayaridhii kabisa.
37 #
Zab 33:9
Ni nani asemaye neno nalo likafanyika,
Ikiwa Bwana hakuliagiza?
38 #
Ayu 2:10
Je! Katika kinywa chake Aliye Juu
Hayatoki maovu na mema?
39 #
Mik 7:9
Mbona anung'unika mwanadamu aliye hai
Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?
40 #
Zab 119:59
Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu,
Na kumrudia BWANA tena.
41 #
Zab 86:4
Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni
Mioyo yetu na mikono.
42 #
Dan 9:5
Sisi tumekosa na kuasi;
Wewe hukusamehe.
43Umetufunika kwa hasira na kutufuatia;
Umeua, wala hukuona huruma.
44Umejifunika nafsi yako kwa wingu,
Maombi yetu yasipite.
45 #
1 Kor 4:13
Umetufanya kuwa takataka, na vifusi
Katikati ya mataifa.
46Juu yetu adui zetu wote
Wametupanulia vinywa vyao.
47Hofu imetujilia na shimo,
Ukiwa na uharibifu.
48Jicho langu lachuruzika mito ya machozi
Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu.
49Jicho langu latoka machozi lisikome,
Wala haliachi;
50 #
Isa 63:15
Hata BWANA atakapoangalia
Na kutazama toka mbinguni.
51Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu,
Kwa ajili ya kuangamizwa kwa binti wa watu wangu.
52 #
Zab 35:7; 69:4 Walio adui zangu bila sababu
Wameniwinda sana kama ndege;
53 #
Yer 37:16; Dan 6:17 Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani,
Na kutupa jiwe juu yangu.
54 #
Zab 69:2
Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu,
Nikasema, Nimekatiliwa mbali.
55 #
2 Nya 33:12; Zab 18:5,6; Yon 2:2 Nililiitia jina lako, BWANA, kutoka lile shimo
Liendalo chini kabisa.
56 #
Zab 6:8; Rum 8:26 Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako
Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.
57 #
Zab 69:18; Isa 58:9; Yak 4:8 Ulinikaribia siku ile nilipokulilia;
Ukasema, Usiogope.
58 #
1 Sam 25:39; Yer 51:36; Zab 35:1; 71:23 Ee BWANA umenitetea katika kisa cha nafsi yangu;
Umeukomboa uhai wangu.
59Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA;
Unihukumie neno langu.
60 #
Yer 11:19
Umekiona kisasi chao chote,
Na mashauri yao yote juu yangu.
61Ee BWANA, umeyasikia matukano yao,
Na mashauri yao yote juu yangu;
62Midomo yao walioinuka juu yangu
Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa.
63 #
Zab 139:2
Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao;
Wimbo wao ndio mimi.
64 #
Zab 28:4; Yer 11:20; 2 Tim 4:14; Ufu 6:10 Utawalipa malipo, Ee BWANA,
Sawasawa na kazi ya mikono yao.
65 #
Zab 8:3
Utawapa ushupavu wa moyo;
Laana yako juu yao.
66Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza
Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA.
Currently Selected:
Maombolezo 3: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Maombolezo 3
3
Upendo wa Mungu huvumilia
1Mimi ni mtu aliyeona mateso
Kwa fimbo ya ghadhabu yake.
2Ameniongoza na kunipeleka katika giza
Wala si katika nuru.
3Hakika juu yangu augeuza mkono wake
Mara kwa mara mchana wote.
4Amechakaza ngozi yangu na nyama yangu;
Ameivunja mifupa yangu.
5Amejenga boma juu yangu,
Na kunizungusha uchungu na uchovu.
6 #
Zab 88:5
Amenikalisha penye giza,
Kama watu waliokufa zamani.
7Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka;
Amenifunga kwa mnyororo mzito.
8 #
Ayu 30:20; Zab 22:2 Naam, nikilia na kuomba msaada,
Huyapinga maombi yangu.
9Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa;
Ameyapotosha mapito yangu.
10 #
Hos 5:14
Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye,
Kama simba aliye mafichoni.
11 #
Hos 6:1
Amezigeuza njia zangu, na kuniraruararua;
Amenifanya ukiwa.
12 #
Ayu 6:4; Zab 34:2 Ameupinda upinde wake,
Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale.
13Amenichoma viuno
Kwa mishale ya podo lake.
14 #
Neh 4:2-4; Zab 22:6,7; Yer 20:7; Mt 27:29-31 Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote;
Wimbo wao mchana kutwa.
15 #
Yer 9:15
Amenijaza uchungu,
Amenikinaisha kwa pakanga.
16 #
Mit 20:17
Amenivunja meno kwa changarawe;
Amenifunika majivu.
17Umeniweka nafsi yangu mbali na amani;
Nikasahau kufanikiwa.
18 #
Zab 31:22
Nikasema, Nguvu zangu zimepotea,
Na tumaini langu kwa BWANA.
19Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu,
Pakanga na nyongo.
20Nafsi yangu ingali ikiyakumbuka hayo,
Nayo imeinama ndani yangu.
21Najikumbusha neno hili,
Kwa hiyo nina matumaini.
22 #
Neh 9:31; Zab 57:10; Mal 3:6 Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,
Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
23 #
Isa 33:2; Ebr 10:23 Ni mpya kila siku asubuhi;
Uaminifu wako ni mkuu.
24 #
Zab 16:5
BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu,
Kwa hiyo nitamtumaini yeye.
25 #
Zab 130:6
BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,
Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
26 #
Zab 37:7
Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA
Na kumngojea kwa utulivu.
27 #
Zab 90:12
Ni vema mwanadamu aichukue nira
Wakati wa ujana wake.
28 #
Yer 15:17
Na akae peke yake na kunyamaza kimya;
Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake.
29 #
Ayu 42:6
Na atie kinywa chake mavumbini;
Ikiwa yamkini liko tumaini.
30 #
Mik 5:1; Mt 5:39 Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake;
Ashibishwe mashutumu.
31 #
Zab 94:14
Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu
Hata milele.
32Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,
Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
33 #
Ebr 12:10
Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.
Wala kuwahuzunisha.
34Wafungwa wote wa duniani
Kupondwa chini kwa miguu,
35Kuipotosha hukumu ya mtu
Mbele zake Aliye Juu,
36 #
Hab 1:13
Na kumnyima mtu haki yake,
Hayo Bwana hayaridhii kabisa.
37 #
Zab 33:9
Ni nani asemaye neno nalo likafanyika,
Ikiwa Bwana hakuliagiza?
38 #
Ayu 2:10
Je! Katika kinywa chake Aliye Juu
Hayatoki maovu na mema?
39 #
Mik 7:9
Mbona anung'unika mwanadamu aliye hai
Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?
40 #
Zab 119:59
Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu,
Na kumrudia BWANA tena.
41 #
Zab 86:4
Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni
Mioyo yetu na mikono.
42 #
Dan 9:5
Sisi tumekosa na kuasi;
Wewe hukusamehe.
43Umetufunika kwa hasira na kutufuatia;
Umeua, wala hukuona huruma.
44Umejifunika nafsi yako kwa wingu,
Maombi yetu yasipite.
45 #
1 Kor 4:13
Umetufanya kuwa takataka, na vifusi
Katikati ya mataifa.
46Juu yetu adui zetu wote
Wametupanulia vinywa vyao.
47Hofu imetujilia na shimo,
Ukiwa na uharibifu.
48Jicho langu lachuruzika mito ya machozi
Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu.
49Jicho langu latoka machozi lisikome,
Wala haliachi;
50 #
Isa 63:15
Hata BWANA atakapoangalia
Na kutazama toka mbinguni.
51Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu,
Kwa ajili ya kuangamizwa kwa binti wa watu wangu.
52 #
Zab 35:7; 69:4 Walio adui zangu bila sababu
Wameniwinda sana kama ndege;
53 #
Yer 37:16; Dan 6:17 Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani,
Na kutupa jiwe juu yangu.
54 #
Zab 69:2
Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu,
Nikasema, Nimekatiliwa mbali.
55 #
2 Nya 33:12; Zab 18:5,6; Yon 2:2 Nililiitia jina lako, BWANA, kutoka lile shimo
Liendalo chini kabisa.
56 #
Zab 6:8; Rum 8:26 Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako
Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.
57 #
Zab 69:18; Isa 58:9; Yak 4:8 Ulinikaribia siku ile nilipokulilia;
Ukasema, Usiogope.
58 #
1 Sam 25:39; Yer 51:36; Zab 35:1; 71:23 Ee BWANA umenitetea katika kisa cha nafsi yangu;
Umeukomboa uhai wangu.
59Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA;
Unihukumie neno langu.
60 #
Yer 11:19
Umekiona kisasi chao chote,
Na mashauri yao yote juu yangu.
61Ee BWANA, umeyasikia matukano yao,
Na mashauri yao yote juu yangu;
62Midomo yao walioinuka juu yangu
Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa.
63 #
Zab 139:2
Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao;
Wimbo wao ndio mimi.
64 #
Zab 28:4; Yer 11:20; 2 Tim 4:14; Ufu 6:10 Utawalipa malipo, Ee BWANA,
Sawasawa na kazi ya mikono yao.
65 #
Zab 8:3
Utawapa ushupavu wa moyo;
Laana yako juu yao.
66Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza
Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA.
Currently Selected:
:
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.