YouVersion Logo
Search Icon

Luka 7

7
Yesu amponya mtumwa wa afisa
1 # Mt 8:5-13 Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.
2 # Yn 4:47 Na mtumwa wake afisa mmoja alikuwa mgonjwa, karibu kufa; naye ni mtu aliyempenda sana. 3Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake. 4Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili; 5maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi. 6Basi Yesu akaenda pamoja nao. Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule afisa alituma rafiki kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari langu; 7kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona. 8Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. 9Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii. 10Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima.
Yesu amfufua mtoto wa mama mjane
11Baadaye kidogo alikwenda mpaka katika mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. 12#Lk 8:42; 1 Fal 17:17 Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wengi mjini walikuwa pamoja naye. 13Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. 14Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. 15#1 Fal 17:23; 2 Fal 4:36 Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. 16#Lk 1:68; 19:44 Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake. 17Habari hii yake ikaenea kote katika Yudea yote, na katika nchi zote za karibu.
Ujumbe kutoka kwa Yohana Mbatizaji
18 # Mt 11:2-19 Wanafunzi wa Yohana wakamletea habari za hayo yote. 19#Zab 40:7; 118:26; Mal 3:1; Dan 9:26 Ndipo Yohana alipowaita wawili katika wanafunzi wake, akawatuma kwa Yesu akiuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? 20Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? 21Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona. 22#Isa 35:5-6; 61:1 Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa Habari Njema. 23Naye heri mtu yeyote asiyechukizwa nami.
24Basi, wajumbe wa Yohana walipokwisha ondoka, alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? 25Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Jueni, watu wenye mavazi ya utukufu, wanaokaa kwa raha, wamo katika majumba ya kifalme. 26#Lk 1:76 Lakini, mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambia, na aliye zaidi ya nabii. 27#Mal 3:1 Huyo ndiye aliyeandikiwa haya,
Tazama, namtuma mjumbe wangu
Mbele ya uso wako,
Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.
28 # Lk 1:15 Nami nawaambia, Katika wale waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana; lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye. 29#Mt 21:32; Lk 3:7,12 Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. 30#Mdo 13:46 Lakini, Mafarisayo na wanasheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye. 31Bwana akasema, Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini? 32Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia. 33#Lk 15:2 Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. 34Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi. 35Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
Mwanamke mwenye dhambi asamehewa
36 # Lk 11:37 Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. 37#Mt 26:7-13; Mk 14:3; Yn 12:3-8 Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. 38#Mt 26:7-13; Yn 12:3-8 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusubusu miguu yake na kuipaka yale marhamu. 39Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi. 40Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mwalimu, nena. 41Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini. 42Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi? 43Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki. 44#Mwa 18:4 Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. 45#Rum 16:16 Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. 46Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. 47Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo. 48#Lk 5:20,21 Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako. 49Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe dhambi? 50#Lk 8:48; 17:19; 18:42 Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, nenda zako kwa amani.

Currently Selected:

Luka 7: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in