Luka UTANGULIZI
UTANGULIZI
Jina la mwandishi wa Injili hii halitajwi katika Injili yenyewe. Lakini kutokana na mapokeo ya Kikristo pamoja na ushuhuda uliomo katika Injili inathibitika kuwa ni Luka ambaye ndiye pia mwandishi wa kitabu cha Matendo ya Mitume (Lk 1:1-4; Mdo 1:1-2).
Luka alikuwa, Mgiriki, mwenyeji wa Antiokia ya Shamu; alikuwa daktari na mtu mwenye ujuzi wa kuandika. Uandishi wake ni safi wenye utaratibu mzuri. Ametumia mbinu za kuitumia historia katika kuandika na kuihakiki imani ya Kikristo tangu mwanzo wake hadi ukristo ulipofika Rumi. Wengi wa wasomi wa Agano Jipya huita Injili hii “kitabu kilicho kizuri kupita vyote duniani”. Ni mwandishi pekee katika Agano Jipya ambaye hakuwa Myahudi. Aliongoka akawa Mkristo na baadaye akaambatana na Paulo katika safari za kushuhudia Injili na kukaa naye kwa muda (Kol 4:14; 2 Tim 4:11; File 24; Mdo 16:10-17; 20:5-16; 21:1-18; 27:1—28:16).
Walengwa wa Injili hii walikuwa Wakristo walioongea Kigiriki. Kwa hiyo, kwa kuwa walengwa hao hawakufahamu vizuri sana desturi, dini na mazingira ya Wayahudi, Luka hakunukuu mambo mengi kutoka Agano la Kale. Tena, pale ambapo ilimbidi kutumia maneno ya Kiebrania, ameyatafsiri hayo katika lugha ya Kigiriki ili yaeleweke vema kwa wasomaji wake (Lk 6:15 rejea Mt 10:4). Katika kukusanya habari za Yesu, Luka ametuachia baadhi ya visa vya kusisimua sana ambavyo haviko katika Injili nyingine: Kwanza kabisa ni habari za kuzaliwa kwake Yohana Mbatizaji na Yesu mwenyewe (sura 1—2); visa vingine vinavyoambatana na safari ya Yesu ya mwisho kwenda Yerusalemu (9:51—18:14) ambamo tuna mengi ya mifano ya kusisimua ya Yesu: Msamaria Mwema (10:25-37), Mwana Mpotevu (15:11-32), Hakimu mbaya (18:1-8) na habari za Mfarisayo na Mtoza ushuru (18:9-14). Visa hivi vitatu vya mwisho ni alama tu ya jinsi Yesu alivyowajali watu ambao hawakubahatika katika jamii. Katika Injili Yesu anawajali sana wanawake na hao walihusika katika huduma yake tangu mwanzo (1:5-56; 2:36-38). Yesu kuwajali sana wanawake (7:11-15,36-50; 8:23; 21:1-4; 24:27-29;), Wasamaria na watu wa mataifa (4:25-27; 10:30-37; 17:11-19). Yesu anawapokea wenye dhambi, fukara, wenye dhiki, wasiojiweza, wenye shida, wajane, waliotengwa kijamii na kidini. Yesu ni rafiki wa wote wanaotubu maana alikuja duniani kutafuta na kuokoa kile kilichopotea (7:36-50; 15:11-32; 18:9-14; 19:1-10; 23:43). Wenye mali nyingi na wenye kujivuna kwa vile hawana dhambi wanaonywa wabadili mwenendo wao, wawe na upendo, wasiwabague wengine (6:24-26; 16:9,19-31).
Currently Selected:
Luka UTANGULIZI: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: