Malaki 3
3
Mjumbe ajaye
1 #
Mdo 7:38; Isa 40:3; 63:9; Hag 2:7; Mt 11:10; Mk 1:2; Lk 1:76; 7:27 Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijia katika hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi. 2#Isa 4:4; Yoe 2:11; Ufu 6:17 Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; 3#Isa 1:25; Zek 13:9; Rum 15:16; 1 Pet 2:5 naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea BWANA dhabihu katika haki. 4Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za BWANA, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani. 5#1 The 1:7; Yak 5:4,8,9 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi. 6#Hes 23:19; Rum 11:29; 1 Sam 15:29; Omb 3:22 Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
7 #
Mdo 7:51; Kum 30:1-4; Isa 55:6,7; Zek 1:3 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
Msimwibie Mungu
8 #
Neh 13:10
Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10#Mit 3:9; 1 Nya 26:20; Mwa 7:11; Law 27:30; Hes 18:21-24; Kum 12:6; 14:22-29; Neh 13:12 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11#Amo 4:9 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. 12#Dan 8:9 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.
13Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani? 14#Ayu 21:14; Sef 1:12; Zab 73:11-13 Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi? 15#Zab 73:12; 95:9 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.
Tuzo la waaminio
16 #
Mwa 22:12; 1 Fal 18:3,12; Zab 33:18; 111:10; Ayu 28:28; Ebr 3:13 Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake. 17Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. 18Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.
Currently Selected:
Malaki 3: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: