Marko 6
6
Kukataliwa kwa Yesu Nazareti
1 #
Mt 13:53-58; Lk 4:15-30 Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata. 2#Yn 7:15 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? 3Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na dada zake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. 4#Yn 4:44 Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. 5#Mk 6:13 Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.
Yesu awatuma wale kumi na wawili
6Akastaajabu kwa sababu ya kutoamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.
7 #
Mt 10:1,9-15; Lk 9:1-6 Akawaita wale Kumi na Wawili, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;#Lk 10:1 8#Lk 10:4-11 akawakataza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa fimbo tu; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za kibindoni; 9lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili. 10Akawaambia, Mahali popote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hadi mtakapotoka mahali pale. 11#Mdo 13:51 Na mahali popote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung'uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu, kuwa ushuhuda kwao. 12Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. 13#Yak 5:14,15 Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaponya.
Kifo cha Yohana Mbatizaji
14 #
Mt 16:14; Mk 8:28; Lk 9:19 Naye Mfalme Herode akasikia habari; kwa maana jina lake lilikuwa limeenea, akasema, Yohana Mbatizaji amefufuka katika wafu, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake.#Lk 3:19,20 15Wengine walisema, Ni Eliya. Wengine walisema, Huyu ni nabii, au ni kama mmoja wa manabii. 16Lakini Herode aliposikia, alisema, Yohana, niliyemkata kichwa, amefufuka.
17 #
Lk 3:19-20
Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo, ndugu yake, kwa kuwa amemwoa; 18#Law 18:16 kwa sababu Yohana alimwambia Herode, Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo. 19Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asiweze. 20Maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha. 21Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya; 22ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lolote utakalo, nitakupa. 23#Est 5:3-6 Akamwapia, lolote utakaloniomba nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu. 24Basi akatoka, akamwuliza mamaye, Niombe nini? Naye akasema, Kichwa cha Yohana Mbatizaji. 25Mara akaingia kwa haraka mbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. 26Mfalme akahuzunika sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia. 27Mara mfalme akatuma askari, akaamuru kuleta kichwa chake. Basi akaenda, akamkata kichwa mle gerezani, 28akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye. 29Wanafunzi wake waliposikia habari, walikwenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.
Kuwalisha watu elfu tano
30 #
Lk 9:10; 10:17 Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote waliyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha. 31Akawaambia, Njooni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula. 32#Mt 14:13-21; Lk 9:11-17; Yn 6:1-13 Wakaenda zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu. 33Watu wakawaona wakienda zao, na wengi wakatambua, wakaenda huko mbio kwa miguu, toka miji yote, wakatangulia kufika. 34#Hes 27:17; 1 Fal 22:17; 2 Nya 18:16; Eze 34:5; Mt 9:36 Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi. 35#Mk 8:1-9 Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; 36uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. 37Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari#6:37 Dinari moja ni ujira wa kazi ya kutwa. mia mbili ili tuwape kula? 38Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili. 39Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi. 40Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini. 41#Mk 7:34 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandalie; na wale samaki wawili akawagawia wote. 42Wakala wote wakashiba. 43#Kum 28:5 Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia. 44Na walioila ile mikate walikuwa wanaume elfu tano.
Yesu atembea juu ya maji
45 #
Mt 14:22-36; Yn 6:15-21 Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, watangulie kwenda ng'ambo hata Bethsaida, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. 46Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.
47Na kulipokuwa jioni mashua ilikuwa katikati ya bahari, na yeye yu peke yake katika nchi kavu. 48Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa unwakabili; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita. 49Nao walipomwona anatembea juu ya bahari, walidhani ya kuwa ni mzuka, wakapiga yowe, 50kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope. 51#Mk 4:39 Akapanda mle katika mashua walimo; upepo ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao; 52kwa maana hawakufahamu habari za ile mikate, lakini mioyo yao ilikuwa mizito.
Kuwaponya wagonjwa Genesareti
53Hata walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti, wakatia nanga. 54Nao wakiisha kutoka mashuani, mara watu walimtambua, 55wakaenda mbio, wakizunguka nchi ile yote, wakaanza kuwachukua vitandani waliokuwa wagonjwa, kwenda kila mahali waliposikia kwamba yupo. 56#Mk 5:27,28; Mdo 5:15; 19:11,12 Na kila alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse angaa pindo la vazi lake; nao wote waliomgusa wakapona.
Currently Selected:
Marko 6: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: