YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 1

1
KITABU CHA KWANZA
Njia mbili
1 # Mwa 5:24; Ayu 31:5; Zab 81:12; Mit 4:14 Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 # Yer 17:8; Mwa 39:3; Zab 128:2 Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.
4Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,
Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
6 # Nah 1:7; Yn 10:14 Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,
Bali njia ya wasio haki itapotea.

Currently Selected:

Zaburi 1: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in