YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 107

107
KITABU CHA TANO
Shukrani kwa kukombolewa katika dhiki
1 # 1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 106:1; 118:1; 136:1; Yer 33:11; Mt 19:17 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2Na waseme hivi waliokombolewa na BWANA,
Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi.
3 # Zab 106:47; Isa 49:12; Yer 29:14; Eze 39:27 Akawakusanya kutoka nchi zote,
Mashariki na magharibi, kaskazini na kusini.
4Walitangatanga jangwani katika njia ya nyika;
Hawakuona mji wa kukaa.
5Waliona njaa na kiu,
Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao.
6 # Zab 50:15; Isa 41:17; Yer 29:12-14; Hos 5:15 Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,
Akawaponya na shida zao.
7 # Ezr 8:21; Isa 63:12 Akawaongoza kwa njia ya kunyoka,
Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa.
8Na wamshukuru BWANA, kwa fadhili zake,
Na maajabu yake kwa wanadamu.
9 # Zab 34:10; Isa 55:1; Mt 5:6; Lk 1:53 Maana hushibisha nafsi yenye shauku,
Na nafsi yenye njaa huijaza mema.
10 # Ayu 36:8 Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti,
Wamefungwa katika taabu na minyororo,
11 # Omb 3:42; Zab 73:24; Lk 7:30; Mdo 20:27 Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu,
Wakalidharau shauri lake Aliye Juu.
12 # Isa 63:5 Hata akawadhili moyo kwa taabu,
Wakajikwaa, wala pasiwe na wa kuwasaidia.
13Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,
Akawaponya kutoka kwa shida zao.
14 # Zab 146:7; Mdo 12:7 Aliwatoa katika giza na uvuli wa mauti,
Akaivunja minyororo yao.
15Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake,
Na maajabu yake kwa wanadamu.
16 # Isa 45:2 Maana ameivunja milango ya shaba,
Ameyakata mapingo ya chuma.
17 # Zab 14:1; Mit 1:22; Omb 3:39 Wapumbavu, kwa sababu ya ukosaji wao,
Na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa.
18Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula,
Wameyakaribia malango ya mauti.
19Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,
Akawaponya kutoka kwa shida zao.
20 # Hes 21:8; 2 Fal 20:4; Mt 8:8 Hulituma neno lake, huwaponya,
Huwatoa katika maangamizo yao.
21Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake,
Na maajabu yake kwa wanadamu.
22 # Law 7:12; Zab 50:14; Ebr 13:15 Na wamtolee dhabihu za kushukuru,
Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba.
23Washukao baharini katika merikebu,
Wafanyao kazi yao katika maji mengi,
24Hao huziona kazi za BWANA,
Na maajabu yake vilindini.
25Maana alisema, akavumisha upepo wa dhoruba,
Ukayainua juu mawimbi ya bahari.
26 # Zab 22:14; Isa 13:7; Nah 2:10 Walirushwa juu mbinguni, waliteremka hadi vilindini,
Uhodari wao ukayeyuka katika maafa yao.
27Waliyumbayumba, walipepesuka kama mlevi,
Ujuzi wao wote uliwaishia.
28Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,
Akawaponya kutoka kwa shida zao.
29 # Zab 65:7; Isa 50:2; Mt 8:26; Mk 4:39-41 Huituliza dhoruba, ikawa shwari,
Mawimbi yake yakanyamaza.
30Ndipo walipofurahi kwa kuwa yametulia
Naye akawaleta mpaka bandani waliyoitamani.
31Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake,
Na maajabu yake kwa wanadamu.
32Na wamtukuze katika kusanyiko la watu,
Na wamhimidi katika baraza la wazee.
33 # 1 Fal 17:1; Isa 34:9,10; Eze 30:12; Yoe 1:20; Nah 1:4 Amegeuza mito ikawa jangwa,
Na chemchemi za maji zikawa nchi kavu.
34 # Mwa 13:10 Nchi ya matunda mengi ikawa uwanda wa chumvi,
Kwa sababu ya uovu wa wakazi wake.
35 # Isa 41:18 Amegeuza jangwa ikawa ziwa la maji,
Na nchi kavu ikawa chemchemi za maji.
36 # Mdo 17:26 Maana amewakalisha huko wenye njaa,
Nao wamejenga mji wa kukaa.
37Wakapanda mbegu katika mashamba,
Na kutia mizabibu iliyotoa matunda yake.
38 # Mwa 12:2 Naye aliwabariki wakaongezeka sana,
Wala hawapunguzi mifugo wao.
39 # 2 Fal 10:32; Ayu 12:21 Walipopungua na kudhilika,
Kwa kuonewa na dhiki na huzuni.
40Aliwamwagia wakuu dharau,
Na kuwazungusha katika nyika isiyo na njia.
41 # 1 Sam 2:8; 2 Sam 7:8; Ayu 8:7 Lakini alimwinua mhitaji juu mbali na mateso,
Na kuwaongeza jamaa zao kama kundi la kondoo.
42 # Ayu 22:19; 5:16; Mit 10:11 Wanyofu wa moyo wanaona na kufurahi,
Na waovu wote wananyamazishwa.
43 # Yer 9:12; Dan 12:10 Aliye na hekima na ayaangalie hayo;
Na wazitafakari fadhili za BWANA.

Currently Selected:

Zaburi 107: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in