Zaburi 138
138
Shukrani na sifa ya Daudi
1 #
Zab 119:46
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
2 #
1 Fal 8:29; Zab 5:7; Dan 6:10; Yon 2:7; Isa 42:21 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,
Nitalishukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umeikuza ahadi yako,
na jina lako juu ya vyote.
3 #
2 Kor 12:9; Zek 10:12 Siku ile niliyokuita uliniitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
4Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru,
Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.
5Naam, wataziimba njia za BWANA,
Kwa maana utukufu wa BWANA ni mkuu.
6 #
Mit 3:34; Yak 4:6 Ingawa BWANA yuko juu, anamjali mnyenyekevu,
Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
7 #
Zab 23:3
Nijapopitia katika shida,
Unanilinda juu ya hasira ya adui zangu,
Unaunyosha mkono wako,
Na mkono wako wa kulia unaniokoa.
8 #
Zab 57:2; Flp 1:6 BWANA atanitimizia malengo yake kwangu;
Ee BWANA, fadhili zako ni za milele;
Usiiache kazi ya mikono yako.
Currently Selected:
Zaburi 138: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

:
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.