YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 147

147
Sifa kwa Mungu kuutunza Yerusalemu
1Haleluya.
Msifuni Bwana;
Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu sifa,
Maana ni mwenye fadhili, na anastahili kuimbiwa sifa.
2 # Kum 30:3; Isa 27:13; Yer 32:37; Eze 36:24 BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu,
Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.
3 # Isa 61:1; Lk 4:18 Huwaponya waliopondeka moyo,
Na kuyaganga majeraha yao.
4 # Mwa 15:5; Isa 40:26 Huihesabu idadi ya nyota,
Huzipa zote majina.
5 # 1 Nya 16:25; Nah 1:3 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu,
Akili zake hazina mpaka.
6 # Zab 146:8 BWANA huwategemeza wenye upole,
Huwaangusha chini wenye jeuri.
7 # Efe 5:20 Mwimbieni BWANA kwa kushukuru,
Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.
8 # Ayu 38:20 Huzifunika mbingu kwa mawingu,
Huitengenezea nchi mvua,
Na kuichipusha nyasi milimani.
9 # Ayu 38:41; Mt 6:26; Lk 12:24 Humpa mnyama chakula chake,
Wana-kunguru waliao.
10 # Hos 1:7 Hapendezwi na nguvu za farasi,
Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji.#147:10 au mtu.
11BWANA huwaridhia wao wamchao,
Na kuzitarajia fadhili zake.
12Msifu BWANA, Ee Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
13Maana amevikaza vipingo vya malango yako,
Amewabariki wanao ndani yako.
14Ndiye aletaye amani mipakani mwako,
Hukushibisha kwa ngano safi.
15 # Ayu 37:12 Huipeleka amri yake juu ya nchi,
Neno lake lapiga mbio sana.
16Ndiye atoaye theluji kama sufu,
Huimwaga barafu yake kama majivu,
17Hutupa mvua ya mawe kama makombo,
Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama?
18Hulituma neno lake na kuviyeyusha,
Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka.
19 # Kum 33:4; Mal 4:4; Rum 3:2 Hulitangaza neno lake kwa Yakobo,
Na amri zake na hukumu zake kwa Israeli.
20 # Kum 4:32; Mdo 14:16; Rum 3:1-2 Hakulitendea taifa lolote mambo kama hayo,
Wala hukumu zake hawakuzijua.
Haleluya.

Currently Selected:

Zaburi 147: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in