Zaburi 36
36
Uovu wa watu na wema wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi, mtumishi wa Bwana
1 #
Rum 3:18; Mwa 20:11; Mit 8:13; Mhu 12:3 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake,
Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.
2Kwa maana hujipendekeza machoni pake
Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.
3 #
Yer 4:22
Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila,
Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.
4 #
Mik 2:1; Isa 65:2 Huwaza maovu kitandani pake,
Hujiweka katika njia mbaya; hauchukii ubaya.
5 #
Zab 57:10
Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni,
Uaminifu wako hadi mawinguni.
6 #
Ayu 11:8; Rum 11:33; Ayu 7:20; Zab 145:9 Haki yako ni kama milima ya Mungu,
Hukumu zako ni vilindi vikuu,
Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama.
7 #
Rut 2:12
Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako!
Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
8 #
Ayu 20:17; Ufu 22:1 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,
Nawe utawanywesha kutoka mto wa furaha zako.
9 #
Isa 12:3; Yer 2:13; Zek 13:1; Yn 4:10,14; Ufu 21:6; Mdo 26:18; Efe 5:8; Kol 1:13; 1 Pet 2:9 Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,
Katika nuru yako tutaona nuru.
10 #
Yer 22:16
Uwadumishie wakujuao fadhili zako,
Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.
11Mguu wa kiburi usinikaribie,
Wala mkono wa wasio haki usinifukuze.
12Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu;
Wameangushwa chini wasiweze kusimama.
Currently Selected:
Zaburi 36: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: