Zaburi 41
41
Hakikisho la msaada wa Mungu na ombi la uponyaji
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Mit 14:21; Mk 10:21 Heri amkumbukaye mnyonge;#41:1 Au maskini.
BWANA atamwokoa siku ya taabu.
2BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,
Naye atafanikiwa katika nchi;
Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.
3BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.
Katika ugonjwa wake unamponya maradhi yake yote.
4 #
Zab 6:2
Nami nilisema, BWANA, unifadhili,
Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.
5Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,
Atakufa lini, jina lake lipotee?
6 #
Zab 12:2
Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,
Moyo wake hujikusanyia maovu,
Naye atokapo nje huyanena.
7Wote wanaonichukia wananong'onezana juu yangu,
Wananiwazia yaliyo mabaya zaidi.
8Wanafikiri pigo liualo limemshika,
Akalala asiweze kusimama tena.
9 #
Mt 26:23; Oba 1:7; Mk 14:18; Lk 22:21; Yn 13:18 Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini,
Aliyekula pamoja nami,
Ameniinulia kisigino chake.
10Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,
Uniinue nipate kuwalipa.
11Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami,
Kwa kuwa adui yangu hajivunii kunishinda.
12 #
Zab 34:15; Mdo 2:28 Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza,
Umeniweka mbele za uso wako milele.
* * *
13 #
Zab 106:48
Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli,
Tangu milele hata milele. Amina na Amina.
KITABU CHA PILI
Currently Selected:
Zaburi 41: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

:
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.