Ufunuo 12
12
Mwanamke na joka
1Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili. 2#Isa 66:7; Mik 4:10 Naye alikuwa ana mimba, akilia, akiwa na uchungu na kuumwa katika kuzaa. 3#Dan 7:7 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. 4#Dan 8:10 Na mkia wake unakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, limle mtoto wake. 5#Isa 66:7; Zab 2:9; Ufu 19:15 Naye akazaa mtoto wa kiume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hadi kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. 6#Mt 2:13; Ufu 11:2,3 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.
Mikaeli amshinda joka
7 #
Dan 10:13,21; 12:1; Yud 1:9 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika wake wakapigana na lile joka, lile joka nalo likapigana nao pamoja na malaika wake; 8lakini hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9#Mwa 3:1,14; Lk 10:18; Yn 12:31; Zek 3:1,2 Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye. 10#Ayu 1:9-11; Zek 3:1; Ufu 11:15; Lk 22:31 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11#Rum 8:37; Ufu 7:14 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 12#Isa 44:23; 49:13 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Joka anapigana tena katika dunia
13Na joka lile lilipoona ya kuwa limetupwa katika nchi, lilimfuatia mwanamke yule aliyemzaa mtoto wa kiume. 14#Dan 7:25; 12:7 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hadi mahali pake, hapo alishwapo kwa nyakati tatu na nusu, mbali na nyoka huyo. 15Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, ili achukuliwe na mto ule. 16Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule lililoutoa lile joka katika kinywa chake. 17#Ufu 13:7; 14:12; 19:10; 1 Yoh 5:10; Mwa 3:15 Joka likamkasirikia yule mwanamke, likaenda zake lifanye vita juu ya wazawa wake waliobakia, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; nalo likasimama juu ya mchanga wa bahari.
Currently Selected:
Ufunuo 12: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: