YouVersion Logo
Search Icon

Warumi 12

12
Maisha mapya katika Kristo
1 # Rum 6:11,13; 1 Pet 2:5; Yn 4:24 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2#Efe 4:23; 5:10,17; Rum 1:28; Gal 1:4 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
3 # 1 Kor 12:11; Efe 4:7 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. 4#1 Kor 12:12 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5#1 Kor 12:27; Efe 4:25 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6#1 Kor 12:4-11 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa ni unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; 7#1 Pet 4:10,11 ikiwa ni huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8#Mt 6:3; 2 Kor 8:2; 9:7 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; msimamizi, na asimamie kwa bidii; anayerehemu, na arehemu kwa furaha.
Sifa za Mkristo
9 # 1 Pet 1:22; 1 Tim 1:5; Amo 5:15 Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema. 10#2 Pet 1:7; Flp 2:3 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; 11#Ufu 3:15; Mdo 18:25 kwa bidii, bila kulegea; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; 12#1 The 5:17 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali; 13#Ebr 13:2 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. 14#Mt 5:44; Lk 6:28; Mdo 7:59; 1 Kor 4:12 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. 15#Zab 35:13 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. 16#Mit 3:7; Rum 15:5; 11:20 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili. 17#Isa 5:21; 1 The 5:15 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. 18#Mk 9:50; Ebr 12:14 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. 19#Kum 32:35; Law 19:18; Mt 5:39; 2 The 1:6,7; Rum 13:4; Ebr 10:30 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. 20#Mit 25:21-22; Mt 5:44 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. 21Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Currently Selected:

Warumi 12: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in