Warumi 3
3
1Basi Myahudi ana nini zaidi? Na kutahiriwa kwafaa nini? 2#Rum 9:4; Kum 4:7,8; Zab 147:19,20; 103:7; 1 Pet 4:11 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. 3#Rum 9:6; 11:29; 2 Tim 2:13 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutoamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? 4#Zab 51:4; 116:11 La hasha! Mungu aonekane kuwa kweli japo kila mtu ni mwongo; kama ilivyoandikwa,
Ili ujulikane kuwa una haki katika maneno yako,
Ukashinde uingiapo katika hukumu.
5Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.) 6Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu? 7Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi? 8#Rum 6:1,2 Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo), Na tufanye mabaya, ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.
Hakuna mwenye haki
9 #
Rum 1:18—2:24
Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wagiriki ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi; 10#Zab 14:1-3; 53:1-3 kama ilivyoandikwa, ya kwamba,
Hakuna mwenye haki hata mmoja.
11Hakuna afahamuye;
Hakuna amtafutaye Mungu.
12Wote wamepotoka, wameoza wote pia;
Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
13 #
Zab 5:9; 140:3 Koo lao ni kaburi wazi,
Kwa ndimi zao wametumia hila.
Sumu ya fira iko chini ya midomo yao.
14 #
Zab 10:7
Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15 #
Isa 59:7-8
Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.
17Wala njia ya amani hawakuijua.
18 #
Zab 36:1
Kumcha Mungu hakupo machoni pao.
19 #
Rum 2:12; Gal 3:22 Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; 20#Zab 143:2; Gal 2:16; Rum 7:7 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
Haki kupitia kwa imani
21 #
Mdo 10:43; Rum 1:17 Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na Torati na Manabii; 22#Gal 2:16 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; 23#Rum 9:19; 5:2 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24#Rum 5:1; Efe 2:8 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 25#Law 16:12-15; Ebr 4:16; Efe 1:7 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho#3:25 Upatanisho hapa maana yake ni, Kiti cha rehema. kwa njia ya imani katika damu yake, ili aoneshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; 26apate kuonesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu.
27 #
1 Kor 1:9,31 Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. 28#Gal 2:16 Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. 29#Rum 10:12 Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; 30#Kum 6:4; Gal 3:20; Rum 4:11,12 kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo. 31#Rum 4:3; 8:4; Mt 5:17 Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? La hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.
Currently Selected:
Warumi 3: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: