YouVersion Logo
Search Icon

Ruthu 4

4
Ndoa ya Boazi na Ruthu
1 # Rut 3:12 Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi. 2#Kut 18:21,22; Kum 16:18; 17:9; 29:10; 1 Fal 21:8; Zab 82:2; Mit 31:23 Kisha akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, Ninyi nanyi, ketini hapa. Wakaketi. 3Kisha akamwambia yule jamaa, Huyu Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi aliyokuwa nayo ndugu yetu, Elimeleki; 4#Yer 32:7,8; Rum 12:17; 2 Kor 8:21; Flp 4:8; Mwa 23:18; Law 25:25 nami ilikuwa nia yangu nikujulishe wewe, na kukuambia, Uinunue mbele ya hawa waliopo na mbele ya wazee wa watu wangu. Kama wewe utaikomboa, haya, uikomboe; lakini kama hutaikomboa, uniambie ili nijue mimi; kwa kuwa hakuna mtu wa kuikomboa ila wewe, na baada yako ni mimi. Naye akasema, Nitaikomboa mimi. 5#Mwa 38:8; Kum 25:5,6; Rut 3:13; Mt 22:24 Ndipo Boazi aliposema, Siku ile utakapolinunua shamba mkononi mwa Naomi, unamnunua Ruthu pia, huyu Mmoabi, mkewe marehemu, ili makusudi umwinulie marehemu jina katika urithi wake. 6#Rut 3:12,13 Basi yule jamaa aliyekuwa wa karibu akasema, Mimi sitaweza kulikomboa kwa nafsi yangu, nisije nikauharibu urithi wangu mwenyewe; basi haki yangu ya kulikomboa ujichukulie wewe, maana mimi sitaweza kulikomboa.
7 # Kum 25:7,9 Basi hii ilikuwa desturi zamani za kale katika Israeli, kwa habari ya kukomboa na kubadilishana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israeli. 8Basi yule jamaa akamwambia Boazi, Wewe ujinunulie mwenyewe. Akavua kiatu chake. 9Naye Boazi akawaambia wale wazee na watu wote, Leo hivi ninyi ni mashahidi ya kwamba mimi nimenunua yote yaliyokuwa ya Elimeleki, na yote yaliyokuwa ya Kilioni na Maloni, mkononi mwa Naomi. 10#Kum 25:5-6 Tena, huyu Ruthu Mmoabi, mkewe Maloni, nimemnunua awe mke wangu, makusudi nipate kumwinulia marehemu jina katika urithi wake, jina lake marehemu lisikatike miongoni mwa ndugu zake, wala langoni pa mji wake; leo hivi ninyi ni mashahidi. 11#Mwa 29:31; Mwa 1:28; 9:1; 17:16; Zab 127:3; 128:3; Kum 25:9; Mwa 35:16; Mik 5:2 Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu. 12#Mwa 38:27-30; 1 Nya 2:4; Mt 1:3; 1 Sam 2:20 Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa BWANA katika mwanamke huyu.
Nasaba ya Daudi
13 # Mwa 29:31; 33:5 Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na BWANA akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume. 14#Lk 1:58; Rum 12:15 Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe BWANA, asiyekuacha leo ukiwa huna jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli. 15#1 Sam 1:8 Naye atakurejeshea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa.
16Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake. 17#Lk 1:58,59 Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi;#4:17 Obedi: Maana yake ni ‘Mtumishi” au “anayehudumu’. yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.
18 # 1 Nya 2:4; Mt 1:3 Hivi ndivyo vizazi vya Peresi; Peresi alimzaa Hesroni; 19na Hesroni akamzaa Ramu; na Ramu akamzaa Aminadabu; 20#Hes 1:7 na Aminadabu akamzaa Nashoni; na Nashoni akamzaa Salmoni; 21na Salmoni akamzaa Boazi; na Boazi akamzaa Obedi; 22na Obedi akamzaa Yese; na Yese akamzaa Daudi.

Currently Selected:

Ruthu 4: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in