Luka 22
22
Mpango wa Kumwua Yesu
(Mt 26:1-5; Mk 14:1-2; Yh 11:47-53)
1Ilikuwa karibu ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, inayoitwa Pasaka. 2Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walitaka kumwua Yesu kwa siri kwa sababu waliogopa kile ambacho watu wangefanya.
Yuda Akubali Kuwasaidia Adui wa Yesu
(Mt 26:14-16; Mk 14:10-11)
3Mmoja wa mitume kumi na wawili wa Yesu aliitwa Yuda Iskariote. Shetani alimwingia Yuda, 4akaondoka, akaenda kuongea na viongozi wa makuhani na baadhi ya wakuu wa askari walinzi wa Hekalu. Aliongea nao kuhusu namna ya kumkabidhi Yesu kwao. 5Makuhani walifurahia sana hili. Wakaahidi kumlipa Yuda pesa ikiwa angefanya hivi. 6Akakubali, kisha alianza kusubiri muda mzuri wa kumkabidhi Yesu kwao. Alitaka kumkabidhi Yesu kwao wakati hakuna kundi la watu ambao wangeona.
Karamu ya Pasaka
(Mt 26:17-25; Mk 14:12-21; Yh 13:21-30)
7Siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu#22:7 Siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu Pasaka. ilifika. Hii ni siku ambayo Wayahudi daima walichinja kondoo kwa ajili ya Pasaka. 8Yesu aliwaambia Petro na Yohana, “Nendeni mkaandae mlo wa Pasaka ili tule.”
9Wakamwambia, “Unataka tukauandae wapi?”
Akawaambia, 10“Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mtu amebeba mtungi wa maji. Mfuateni. Ataingia katika nyumba. 11Mwambieni mmiliki wa nyumba, ‘Mwalimu anakuomba tafadhali utuoneshe chumba ambacho yeye na wafuasi wake wanaweza kulia mlo wa Pasaka.’ 12Mmiliki atawaonesha chumba kikubwa ghorofani kilicho tayari kwa ajili yetu. Andaeni mlo humo.”
13Hivyo Petro na Yohana wakaondoka. Kila kitu kilitokea kama Yesu alivyosema. Na hivyo wakauandaa mlo wa Pasaka.
Chakula cha Bwana
(Mt 26:26-30; Mk 14:22-26; 1 Kor 11:23-25)
14Wakati ulifika kwa wao kula mlo wa Pasaka. Yesu na mitume walikuwa wamekaa pamoja kuzunguka meza ya chakula. 15Yesu akawaambia, “Nilitaka sana kula mlo huu wa Pasaka pamoja nanyi kabla sijafa. 16Sitakula mlo mwingine wa Pasaka mpaka itakapopewa maana yake kamili katika ufalme wa Mungu.”
17Kisha Yesu akachukua kikombe kilichokuwa na divai. Akamshukuru Mungu, na akasema, “Chukueni kikombe hiki na kila mmoja anywe. 18Sitakunywa divai tena mpaka Ufalme wa Mungu utakapokuja.”
19Kisha akaichukua baadhi ya mkate na akamshukuru Mungu. Akaigawa vipande vipande, akawapa vipande mitume na kusema, “Mkate huu ni mwili wangu ninaoutoa kwa ajili yenu. Kuleni kwa kunikumbuka.” 20Katika namna ile ile, baada ya kula chakula, Yesu akachukua kikombe chenye divai na akasema, “Divai hii inawakilisha Agano Jipya kutoka kwa Mungu kwa watu wake. Litaanza pale damu yangu itakapomwagika kwa ajili yenu.”#22:20 Nakala chache za Kiyunani hazina maneno ya Yesu katika sehemu ya mwisho ya mstari wa 19 na mstari wote wa 20.
Nani Atamsaliti Yesu?
21Yesu akasema, “Lakini hapa mezani kuna mkono wa yule atakayenisaliti kwa adui zangu. 22Mwana wa Adamu atakufa kama Mungu alivyoamua. Lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Adamu ili auawe.”
23Ndipo mitume wakaulizana, “Ni nani miongoni mwetu atafanya hivyo?”
Iweni Kama Mtumishi
24Baadaye, mitume wakaanza kubishana kuhusu nani miongoni mwao alikuwa mkuu. 25Lakini Yesu akawaambia, “Wafalme wa mataifa wanawatawala watu kama watumwa wao, na wenye mamlaka juu ya wengine wanataka kuitwa, ‘Wafadhili Wakuu’. 26Lakini ni lazima msiwe hivyo. Aliye na mamlaka zaidi miongoni mwenu lazima awe kama asiye na mamlaka. Anayeongoza anapaswa kuwa kama anayetumika. 27Nani ni mkuu zaidi: Yule anayetumika au yule aliyekaa mezani na kuhudumiwa? Kila mtu hudhani ni yule aliyekaa mezani akihudumiwa, sawa? Lakini nimekuwa pamoja nanyi kama ninayetumika.
28Na ninyi ndiyo mliobaki pamoja nami katika mahangaiko mengi. 29Hivyo ninawapa mamlaka kutawala pamoja nami katika ufalme ambao Baba yangu amenipa. 30Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme huo. Mtakaa katika viti vya enzi na kuwahukumu makabila kumi na mbili ya Israeli.
Yesu Asema Petro Atamkana
(Mt 26:31-35; Mk 14:27-31; Yh 13:36-38)
31Shetani ameomba ili awapepete kwa nguvu kama mkulima anavyopepeta ngano kwenye ungo ili mwanguke. Simoni, Simoni,#22:31 Simoni Jina jingine la Simoni lilikuwa Petro. 32nimekuombea ili usipoteze imani yako! Wasaidie ndugu zako kuwa imara utakaponirudia.”
33Lakini Petro akamwambia Yesu, “Bwana, niko tayari kufungwa gerezani pamoja nawe. Hata kufa pamoja nawe!”
34Lakini Yesu akasema, “Petro, asubuhi kabla jogoo hajawika, utakuwa umenikana mara tatu.”
Iweni Tayari kwa Matatizo
35Kisha Yesu akawaambia mitume, “Kumbukeni nilipowatuma bila pesa, mkoba, wala viatu. Je! mlipungukiwa chochote?”
Mitume wakajibu, “Hapana.”
36Yesu akawaambia, “Lakini sasa kama una pesa au mkoba, uchukue pamoja nawe. Kama huna upanga, uza koti lako ukanunue. 37Maandiko yanasema, ‘Alidhaniwa kuwa mhalifu.’#Isa 53:12 Maandiko haya lazima yatimizwe. Yaliyoandikwa kuhusu mimi yanatimilika sasa.”
38Wafuasi wakasema, “Tazama Bwana, hapa kuna panga mbili.”
Yesu akawaambia, “Nyamazeni, acheni mazungumzo ya namna hiyo!”
Yesu Aomba Akiwa Peke Yake
(Mt 26:36-46; Mk 14:32-42)
39-40Yesu akaondoka mjini akaenda Mlima wa Mizeituni. Wafuasi wake wakaenda pamoja naye. (Alikuwa akienda huko mara kwa mara.) Akawaambia wafuasi wake, “Ombeni ili mtiwe nguvu msije mkajaribiwa.”
41Kisha Yesu akaenda kama hatua hamsini mbali nao. Akapiga magoti na akaomba akisema, 42“Baba, ukiwa radhi, tafadhali usinifanye ninywe katika kikombe#22:42 kikombe Kikombe ni ishara ya mateso. Yesu alitumia dhana ya kukinywea kikombe akimaanisha kuyakubali mateso ambayo angeyapata katika matukio ya kutisha ambayo yangetokea muda mfupi ujao. hiki. Lakini fanya unalotaka wewe, siyo ninalotaka mimi.” 43Kisha malaika kutoka mbinguni akaja akamtia nguvu. 44Yesu aliomba kwa nguvu zaidi na kustahimili zaidi kama mpiganaji wa mieleka akiwa katika mapambano makali. Jasho kama matone ya damu likadondoka kutoka kwenye uso wake.#22:44 Nakala zingine za Kiyunani hazina mstari wa 43 na 44. 45Alipomaliza kuomba, alikwenda kwa wafuasi wake. Akawakuta wamelala, wamechoka kwa sababu ya huzuni. 46Yesu akawaambia, “Kwa nini mnalala? Amkeni, ombeni mtiwe nguvu msije mkajaribiwa.”
Yesu Akamatwa
(Mt 26:47-56; Mk 14:43-50; Yh 18:3-11)
47Yesu alipokuwa anaongea, kundi likaja. Lilikuwa linaongozwa na Yuda, mmoja wa mitume kumi na wawili. Akamwendea Yesu ili ambusu.
48Lakini Yesu akamwambia, “Yuda unatumia busu la urafiki kumsaliti Mwana wa Adamu kwa adui zake?” 49Wafuasi wa Yesu walikuwa wamesimama pale pia. Walipoona kilichokuwa kinatokea, wakamwambia Yesu, “Bwana, tutumie panga zetu?” 50Na mmoja wao akautumia upanga wake. Akakata sikio la kulia la mtumishi wa kuhani mkuu.
51Yesu akasema, “Acha!” Kisha akaligusa sikio la mtumishi na akamponya.
52Yesu akaliambia lile kundi lililokuja kumkamata. Walikuwa viongozi wa makuhani, viongozi wa wazee wa Kiyahudi na askari walinzi wa Hekalu. Akawaambia, “Kwa nini mmekuja hapa mkiwa na mapanga na marungu? Mnadhani mimi ni mhalifu? 53Nilikuwa pamoja nanyi kila siku katika eneo la Hekalu. Kwa nini hamkujaribu kunikamata pale? Lakini sasa ni wakati wenu, wakati ambao giza linatawala.”
Petro Amkana Yesu
(Mt 26:57-58,69-75; Mk 14:53-54,66-72; Yh 18:12-18,25-27)
54Walimkamata Yesu na kumpeleka nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro alimfuata Yesu lakini alikaa nyuma kwa mbali. 55Baadhi ya watu walikoka moto katikati ya ua kisha wakaketi pamoja. Petro naye aliketi pamoja nao. 56Kutokana na mwanga wa moto, mtumishi wa kike alimwona Petro amekaa pale. Akamtazama Petro usoni kwa makini. Kisha akasema, “Huyu pia alikuwa na yule mtu.”
57Lakini Petro akasema si kweli. Akasema, “Mwanamke, simfahamu mtu huyo!” 58Muda mfupi baadaye, mtu mwingine akamwona Petro na akasema, “Wewe pia ni mmoja wa lile kundi!”
Lakini Petro akasema, “Wewe, mimi si mmoja wao!”
59Baada ya kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasema, “Ni kweli, nina uhakika mtu huyu alikuwa pamoja naye, kwa sababu yeye pia anatoka Galilaya.”
60Lakini Petro akasema, “Wewe, wala sijui unazungumza kuhusu nini!”
Alipokuwa bado anazungumza, jogoo aliwika. 61Bwana aligeuka akamtazama Petro kwenye macho yake. Kisha Petro akakumbuka Bwana alivyokuwa amesema ya kwamba, “Kabla ya jogoo kuwika asubuhi, utakuwa umenikana mara tatu.” 62Kisha Petro akatoka nje na kulia kwa uchungu.
Walinzi Wamdhalilisha Yesu
(Mt 26:67-68; Mk 14:65)
63Walinzi waliokuwa wanamlinda Yesu walimfanyia mizaha na kumpiga. 64Wakayafunika macho yake ili asiwaone. Kisha wakampiga na wakasema, “Tabiri, tuambie nani amekupiga!” 65Walimtukana pia matusi ya kila aina.
Yesu Akiwa Mbele ya Viongozi wa Kidini
(Mt 26:59-66; Mk 14:55-64; Yh 18:19-24)
66Alfajiri, viongozi wazee wa watu, viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikusanyika. Walimpeleka Yesu kwenye baraza lao kuu. 67Wakamwambia, “Tuambie ikiwa wewe ni Masihi.”
Yesu akawaambia, “Hamtaniamini ikiwa nitawaambia kuwa mimi ni Masihi. 68Na ikiwa nitawauliza swali, hakika mtakataa kunijibu. 69Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu atakaa upande wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.”
70Wote wakasema, “Kwa hiyo wewe ni Mwana wa Mungu?” Akawajibu, “Mnaweza kusema kuwa mimi ni Mwana wa Mungu.”
71Wakasema, “Je! tunahitaji mashahidi wengine zaidi? Sote tumesikia alichosema yeye mwenyewe!”
Currently Selected:
Luka 22: TKU
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Toleo la Awali
© 2017 Bible League International

: