Mwanzo 10
10
Wazao wa Noa
1Nyuma ya mafuriko ya maji, Semu, Hamu na Yafeti, wana wa Noa, walipata watoto wanaume na wanawake. Hawa ndio wazao wao:
2Wana wa Yafeti walikuwa Gomeri, Magogi, Madayi, Yavani, Tubali, Meseki na Tirasi. 3Wana wa Gomeri walikuwa Askenazi, Rifati na Togarma. 4Wana wa Yavani walikuwa Elisa, Tarsisi, Kitimu na Rodanimu. 5Kutokana na hawa visanga vya watu wa mataifa mengine vikagawanywa kwa inchi zao, kila watu kwa luga yao, kwa jamaa zao, kufuatana na mataifa yao.
6Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misiraimu, Puti na Kanana. 7Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabuta, Rama na Sabuteka. Wana wa Rama walikuwa Seba na Dedani. 8Kushi alikuwa baba ya Nimurodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza katika dunia. 9Alikuwa mwindaji shujaa mbele ya Yawe, ndiyo maana kuna musemo unaosema: “Kama vile Nimurodi mwindaji shujaa mbele ya Yawe.” 10Miji ya kwanza ya utawala wake ilikuwa Babeli, Ereki, na Akadi katika inchi ya Sinari. 11Kutoka kule, Nimurodi alikwenda Asuria, akajenga miji ya Ninawe, Rehoboti-Iri, Kala na 12Reseni unaokuwa kati ya Ninawe na muji mukubwa wa Kala.
13Misiraimu alikuwa babu ya Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanafutuhi, 14Wapatirusi, Wakasiluhi (ambao ndio shina ya Wafilistini), na Wakafutorimu.
15Kanana alikuwa babu ya Sidona, muzaliwa wake wa kwanza, na Heti, 16na vilevile babu ya Wayebusi, Waamori, Wagirgasi, 17Wahivi, Waarki, Wasini, 18Waarwadi, Wazemari na Wahamati. Na nyuma watu wa jamaa mbalimbali za Kanana wakatawanyika, 19hata eneo la inchi yao likakuwa toka Sidona kuelekea upande wa kusini, kuendelea Gerari mpaka Gaza, na kuelekea upande wa mashariki liliendelea kwa Sodoma na Gomora, Adima na Seboimu mpaka Lasa. 20Hao ndio wazao wa Hamu kufuatana na makabila yao, luga zao, inchi zao na mataifa yao.
21Semu, mukubwa wa Yafeti, alikuwa baba ya Waebrania wote. 22Wana wa Semu walikuwa Elamu, Asuri, Aripakisadi, Ludi na Aramu. 23Wana wa Aramu walikuwa Usi, Huli, Geteri na Masi. 24Aripakisadi alizaa Sela, Sela akazaa Eberi. 25Eberi alikuwa na wana wawili: wa kwanza akamwita Pelegi kwa sababu wakati ule watu katika dunia waligawanyika na wa pili akamwita Yokitani. 26Yokitani alikuwa baba ya Almodadi, Selefu, Hazarimaweti, Yera, 27Hadoramu, Uzali, Dikela, 28Obali, Abimaeli, Seba, 29Ofiri, Havila na Yobabu. Hao wote walikuwa wana wa Yokitani. 30Inchi walimokaa ilienea toka Mesa mpaka Sefari katika inchi ya vilima vya upande wa mashariki. 31Hao ndio wazao wa Semu, kufuatana na makabila yao, luga zao, inchi zao na mataifa yao.
32Hao ndio jamaa za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao na mataifa yao. Kutokana nao, mataifa yote yalienea katika dunia nyuma ya mafuriko ya maji.
Currently Selected:
Mwanzo 10: SWC02
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

: