Yoane 13:4-5
Yoane 13:4-5 SWC02
Basi Yesu akaondoka kwenye chakula, akavua kanzu yake, akajifunga kitambaa katika kiuno. Kisha akatia maji ndani ya bakuli, na kuanza kunawisha miguu ya wanafunzi wake na kuipanguza na kile kitambaa alichokifunga katika kiuno.