Yoane 20
20
Kufufuka kwa Yesu
(Mat 28.1-8; Mk 16.1-8; Lk 24.1-12)
1Siku ya kwanza ya juma#20.1 Siku ya kwanza ya juma: Ang. Matayo 28.1 na maelezo yake. asubui mapema, kulipokuwa kungali giza, Maria wa Magdala akaenda kwenye kaburi. Alipofika kule akaona kama jiwe lililofunika kaburi limeondolewa. 2Basi akaenda mbio kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine aliyependwa na Yesu na kuwaambia: “Wameondoa maiti ya Bwana toka katika kaburi na hatujui pahali walipoiweka.”
3Basi Petro na yule mwanafunzi mwingine wakaondoka na kwenda kwenye kaburi. 4Wakaenda mbio wakikimbia wote wawili pamoja, lakini yule mwanafunzi alikimbia mbio zaidi kuliko Petro, akamutangulia kwenye kaburi. 5Yeye akainama na kuchungulia ndani yake, akaona vitambaa vimewekwa pembeni, lakini hakuingia. 6Kisha Simoni Petro akafika nyuma yake na kuingia ndani ya kaburi. Akaona vitambaa vimewekwa pembeni, 7vilevile akaona kitambaa kilichofunika kichwa cha Yesu. Kitambaa kile hakikuwekwa pamoja na vile vingine, lakini kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa peke yake pahali pengine. 8Halafu yule mwanafunzi mwingine aliyetangulia kwenye kaburi akaingia vilevile. Akapata kujionea na kuamini. 9(Ilikuwa vile kwa maana wanafunzi walikuwa hawajaelewa bado Maandiko Matakatifu yanayosema kwamba Yesu anapaswa kufufuka.) 10Kisha mambo hayo hawa wanafunzi wawili wakarudi kwao.
Yesu anamutokea Maria wa Magdala
(Mat 28.9-10; Mk 16.9-11)
11Maria alikuwa akisimama inje karibu na kaburi, akilia. Alipokuwa akilia, akainama na kuangalia ndani ya kaburi, 12akaona wamalaika wawili wanaovaa nguo nyeupe wakiikaa pahali maiti ya Yesu ilipowekwa. Mumoja alikuwa kwa upande wa kichwa na mwingine upande wa miguu. 13Wale wamalaika wakamwuliza: “Ee mama, kwa sababu gani unalia?”
Naye akawajibu: “Kwa sababu wameondoa maiti ya Bwana, nami sijui pahali walipoiweka.”
14Alipokwisha kusema maneno haya, akageuka nyuma, akamwona Yesu akisimama pale, lakini hakutambua kwamba ni yeye. 15Yesu akamwuliza: “Mama, kwa sababu gani unalia? Unamutafuta nani?”
Maria akizani kwamba ni mulimaji wa bustani, akamwambia: “Bwana, kama ni wewe uliyeondoa maiti yake, uniambie pahali ulipoiweka, nami nitakwenda kuitwaa.”
16Yesu akamwambia: “Maria!”
Naye akageuka, akasema kwa kiebrania: “Raboni,” maana yake “Mwalimu.”
17Yesu akamwambia: “Usinishike, kwa sababu sijapanda bado kwa Baba. Lakini kwenda kwa wandugu zangu na kuwaambia kwamba ninapanda kwa Baba yangu anayekuwa Baba yenu vilevile, anayekuwa Mungu wangu na Mungu wenu vilevile.”
18Basi Maria wa Magdala akaenda kuwapasha wanafunzi habari kama amemwona Bwana, na kwamba amemwambia maneno hayo.
Yesu anawatokea wanafunzi wake
(Mat 28.16-20; Mk 16.14-18; Lk 24.36-49)
19Magaribi ya ile ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi walikusanyika katika nyumba na milango ilikuwa imefungwa, kwa sababu waliwaogopa wakubwa wa Wayuda. Mara moja Yesu akawatokea na kusimama katikati yao, akawaambia: “Amani kwenu!” 20Kisha kusema hivi, Yesu akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wanafunzi wakafurahi wakati walipomwona Bwana. 21Yesu akawaambia tena: “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma, mimi ninawatuma ninyi vilevile.” 22Alipokwisha kusema maneno haya, akawapulizia pumzi na kuwaambia: “Mupokee Roho Mutakatifu. 23Watu wote mutakaowasamehe zambi, watasamehewa; nao wote musiowasamehe, hawatasamehewa.”
Yesu na Toma
24Lakini Toma, anayeitwa “Pacha,” aliyekuwa mumoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, hakukuwa pamoja nao wakati Yesu alipokuja. 25Wanafunzi wengine wakamwambia: “Tumemwona Bwana.”
Lakini Toma akawajibu: “Nisipoona alama za misumari katika mikono yake na kutia kidole changu katika kovu za misumari ile, nami nisipoingiza vidole vyangu ndani ya ubavu wake, sitaamini.”
26Ilipotimia juma moja nyuma ya pale, wanafunzi wa Yesu wakakusanyika tena ndani ya nyumba ile ile, na mara hii Toma alikuwa pamoja nao. Ijapokuwa milango ilikuwa imefungwa, Yesu akawatokea tena, akasimama katikati yao na kusema: “Amani kwenu!” 27Kisha akamwambia Toma: “Ujongeze kidole chako hapa na uione mikono yangu; unyooshe mukono wako na kugusa ndani ya ubavu wangu. Usikuwe tena na mashaka, lakini uamini.”
28Toma akamujibu: “Bwana wangu na Mungu wangu!”
29Na Yesu akamwambia: “Umeamini kwa sababu umeniona? Heri wale wanaoamini pasipo kuona!”
Kusudi la kitabu hiki
30Yesu alionyesha vitambulisho vingine vingi mbele ya wanafunzi wake visivyoandikwa katika kitabu hiki. 31Lakini hii imeandikwa kusudi mupate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mupate uzima katika jina lake.
Currently Selected:
Yoane 20: SWC02
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

: