Kutoka 29:45-46
Kutoka 29:45-46 SCLDC10
Nitaishi kati ya Waisraeli, nami nitakuwa Mungu wao. Hapo ndipo watakapotambua kuwa mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili niishi kati yao. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.