Luka 8:47-48
Luka 8:47-48 SCLDC10
Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponywa mara moja. Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda na amani.”