Mattayo MT. 13
13
1SIKU ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari. 2Wakamkusanyikia watu wengi, hatta akapanda chomboni, akaketi; na mkutano wote wakasimama pwani. 3Akasema nao mengi kwa mifano, akinena, Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu. 4Hatta alipokuwa akipanda, nyingine zikaanguka njiani, ndege wakaja wakazila: 5nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa udongo mwingi: marra zikaota, kwa kuwa na udongo haba; 6na jua lilipozuka zikanyauka; na kwa kuwa hazina mizizi zikakauka. 7Nyingine zikaanguka penye miiba; miiba ikamea, ikazisonga: 8nyingine zikaanguka penye udongo mwema, zikazaa, hizi mia, hizi sittini, hizi thelathini. 9Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.
10Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano? 11Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa. 12Kwa maana ye yote aliye na mali atapewa, na hado atazidishiwa tele: lakini ye yote asiye nayo, hatta ile aliyo nayo ataondolewa.
13Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawatazami na wakisikia hawasikii, wala hawafahamu. 14Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likinena,
Kusikia mtasikia, wala hamtafahamu;
Mkitazama mtatazama, wala hamtaona:
15Maana moyo wa watu hawa umekuwa mzito,
Na kwa masikio yao hawasikii vema,
Na macho yao wameyafumba;
Wasije wakaona kwa macho yao
Wakasikia kwa masikio yao,
Wakafahama kwa mioyo yao,
Wakaongoka,
Nikawaponya.
16Lakini ya kheri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. 17Kwa maana amin, nawaambieni, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasivaone; na kuyasikia mnayoyasikia, wasiyasikie. 18Bassi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi. 19Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani. 20Nae aliyepandwa penye miamba, huyu ndiye alisikiae lile neno, akalipokea marra kwa furaha; 21lakini hana mizizi udani yake, hukaa muda mchache; ikitukia shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa. 22Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai. 23Nae aliyepandwa penye udongo mwema, huyu ndive alisikiae lile neno, na kulifahamu; yeye ndiye azaae matunda, huyu mia, na huyu sittini, na huyu thelathini.
24Akawatolea mfano mwingine, akinena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake: 25lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya nganu, akaenda zake. 26Baadae majani ya nganu yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. 27Watumishi wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? limepatapi bassi magugu? 28Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumishi wakamwambia, Bassi, wataka twende tukayakusanye? 29Akasema, La; labuda wakati wa kukusanya magugu, mtangʼoa na nganu pamoja nayo. 30Viacheni vyote vikue hatta wakati wa mavuno: na wakati wa mavuno nitawaambia wavimao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita, mkayachome; bali nganu ikusauyeni ghalani mwangu.
31Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya kharadali, aliyotwati mtu akaipanda katika shamba lake; 32nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, ni kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hatta ndege za anga huja na kutua katika matawi yake.
33Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke, akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia.
34Haya yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; na pasipo mfano hakuwaambia neno: 35illi litimizwe neno lililonenwa mi nabii, akisema,
Nitafunua kinywa changu kwa mifano,
Nitatoa mambo yaliyostirika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.
36Kisha Yesu akawaacha makutano, akaingia nyumbani: wanafunzi wake wakamwendea, wakinena, Tufafanulie mfano wa magugu ya konde. 37Akajibu, akasema, Azipandiie zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; 38na lile konde ni ulimwengu; na zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; 39na yule adui aliyeyapanda ni shetani; na mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika. 40Bassi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii. 41Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya katika ufalme wake machukizo yote, nao watendao maasi, 42na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. 43Ndipo wenye haki watangʼaa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.
44Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyostirika katika shamba; mtu akaiona, akaificha; na kwa furaha yake akaenda akanza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. 45Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mfanya biashara, afafutae lulu nzuri: 46nae alipoona lulu moja ya thamani kubwa, akaenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.
47Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya za killa namna: 48hatta lilipojaa, wakalipandisha pwani; wakaketi, wakakusanya zilizo njema vyomboni, bali zilizo mbaya wakazitupa. 49Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia: malaika watatokea, watawatenga waovu na wenye haki, 50na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.
51Yesu aliwaambia, Mmeyafahamu haya yote? Wakamwambia, Naam, Bwana. 52Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.
53Ikawa Yesu alipomaliza mifano hii, akatoka, akaenda zake. 54Na alipofika inchi yake, akawafundisha katika sunagogi yao, hatta wakashangaa, wakanena, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii? 55Huyu si mwana wa sermala? mama yake sio yeye aitwae Mariamu? Na ndugu zake Yakobo, na Yose, na Simon, na Yuda? 56na maumbu yake, wote hawako kwetu? Bassi huyu amepata wapi haya yote? 57Wakachukizwa nae. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika inchi yake mwenyewe, na nyumbani mwake mwenyewe. 58Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.
Currently Selected:
Mattayo MT. 13: SWZZB1921
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: