YouVersion Logo
Search Icon

Mattayo MT. 15

15
1NDIPO waandishi na Mafarisayo toka Yerusalemi wakamwendea Yesu wakinena, 2Mbona wanafunizi wako huyakhalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. 3Akajibu, akawaambia, Mbona na ninyi huikhalifu amri ya Mungu kwa mapokeo yenu? 4Kwa kuwa Mungu aliamuru, akisema, Mheshimu baba yako na mama yako; na, Amtukanae baba yake au mama yake na afe. 5Bali ninyi hunena, Afakaemwambia baba yake au mama yake, Cho chote kikupasacho kufaidiwa nami ni sadaka, asimheshimu baba yake au mama yake, huwa bassi. 6Mkalitangua neno la Mungu kwa mapokeo yemi. 7Enyi wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya katika khabari zenu, akinena,
8Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao,
Na kwa midomo yao huniheshimu;
Bali mioyo yao iko mbali yangu.
9Nao waniabudu ibada ya burre.
Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wana Adamu.
10Akawaita makutano akawaambia, Sikieni, mfahamu: 11Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho najis mwana Adamu; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho najis mwana Adamu. 12Ndipo wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa? 13Akajibu, akasema, Killa pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni, litangʼolewa. 14Waacheni hawo; ni vipofu, viongozi wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumhukia shimoni wote wawili. 15Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo. Yesu akasema, 16Hatta na ninyi mngali hamna akili? 17Hamjafahamu bado ya kuwa killa kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? 18Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo najis mwana Adamu. 19Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, mauaji, mazini, asharati, uizi, ushuhuda wa uwongo, na matukano; 20hayo ndiyo yamtiayo najis mwana Adamu; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mwana Adamu najis.
21Yesu akatoka huko, akaenda pande za Turo na Sidon. 22Na mwanamke Mkauanaya wa mipaka ile akatokea, akampaazia sauti, akinena, Unirehemu. Bwana, Mwana wa Daud; binti yangu amepagawa sana na pepo. 23Nae hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakinena. Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. 24Nae akajibu, akasema, Sikupelekwa illa kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli. 25Nae akaja akamsujudia, akinena. Bwana, nisaidie. 26Akajibu akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. 27Akasema, Ndio, Bwana, illakini hatta mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. 28Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Ee mwanamke, imani yako kubwa; pata utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
29Yesu akapita huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko. 30Wakamwendea makutano mengi walio na viwete, vipofu, bubu, vilema, na wengine wengi pamoja nao, wakawaweka miguuni pa Yesu; akawaponya; 31hatta makutano wakastaajabu, walipowaona bubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.
32Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia makutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, hawana kitu cha kula: na kuwaaga wakifunga sitaki, wasije wakazimia njiani. 33Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hatta kushibisha makutano mengi namna hii? 34Yesu akawaambia, Mikate mingapi mnayo? Wakasema, Saba, na visamaki vichache. 35Akawaagiza makutano waketi chini: 36akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru, akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano. 37Wakala wote wakashiba: wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, makanda saba, yamejaa. 38Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto. 39Akawaaga makutano, akapanda chomboni, akaenda pande za Magdala.

Currently Selected:

Mattayo MT. 15: SWZZB1921

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in