Mattayo MT. 21
21
1HATTA walipokaribia Yerusalemi, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu akatuma wanafunzi wawili, 2akiwaambia, Enendeni zenu hatta kijiji kile kinachowakabili, na marra mtaona punda amefungwa, na mwana punda pamoja nae: mfungueni mkaniletee. 3Na kama mtu akiwaambieni neno, semeni, Bwana ana haja nao; na marra moja atawapeleka.
4Haya yote yamepata kuwa, illi litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,
5Mwambieni binti Sayuni,
Tazama, mfalme wako anakuja kwako,
Mpole, amepanda punda,
Na mwana punda, mtoto wa punda.
6Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, 7wakamleta yule punda na mwana punda, wakaweka nguo zao juu yao, wakamketisha. 8Watu wengi katika makutano wakatandaza nguo zao njiani; wengine wakikata matawi ya miti, wakiyatandaza njiani. 9Na makutano waliotangulia, na waliofuata, wakapaaza sauti zao, wakinena, Utuokoe sasa, Mwana wa Daud; amebarikiwa ajae kwa jina la Bwana; Utuokoe sasa wewe uliye juu. 10Hatta alipoingia Yerusalenn, mji wote ukataharuki, nkinena, Ni nani huyu? 11Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya.
12Yesu akaingia ndani ya hekalu la Mungu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; 13akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakwitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi. 14Vipofu na viwete wakamwendea hekaluni, akawaponya. 15Lakini makuhani wakuu na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto wakipaaza sauti zao hekaluni, wakinena, Utuokoe sasa, mwana wa Daud! wakakasirika, 16wakamwambia, Wasikia hawa wanenavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa? 17Akawaacha, akatoka nje ya mji mpaka Bethania, akalala huko.
18Hatta assubuhi alipokuwa akirudi mjini, akashikwa na njaa. 19Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake illa majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hatta milele. Mtini ukauyauka marra moja. 20Wanafunzi wake walipoona, wakastaajabu, wakinena, Umenyaukaje mtini marra moja? 21Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambieni, Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hatta mkiuambia mlima huu, Ngʼoka, ukatupwe baharini, itatendeka. 22Na yo yote mtakayoyaomba katika kusali, mkiamini, mtapokea.
23Hatta alipokwisha kuingia hekaluni, makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakinena, Kwa mamlaka gani unafanya haya? Na nani aliyekupa mamlaka haya? 24Yesu akajibu, akawaambia, Nami nitawaulizeni neno moja; mkinijibu, nami nitawaambieni, kwa mamlaka gani ninafanya haya.
25Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wana Adamu? Wakasemezana wao kwa wao, wakinena, Tukisema, Ulitoka mbinguni; atatuambia, Mbona bassi hamkumwamini? 26Na tukisema, Kwa wana Adamu; twaogopa makutano; maana watu wote wanaona ya kuwa Yohana ni nabii. 27Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Nae akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi kwa mamlaka gani ninafanya haya. 28Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo enenda kufanya kazi katika shamba langu la mizabibu. 29Akajibu akasema, Sitaki; baadae akatubu, akaenda. 30Akamwendea yule wa pili, akasema vilevile. Nae akajibu akasema, Nakwenda, Bwana: asiende. 31Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. 32Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na makahaha walimwamini: nanyi mlipoona, hamkutuhu haada ya haya, na kumwamini. 33Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, nae alipanda mizabibu, akazungusha uzio, akachimba shimo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. 34Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumishi wake kwa wale wakulima, wajiokee matunda yake. 35Wale wakulima wakawakamata watumishi wake, huyu wakampiga, na mwingine wakamwua, na mwingine wakampiga mawe. 36Akatuma tena watumishi wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawatenda vilevile. 37Baadae akamtuma mwanawe kwao, akinena, Mwana wangu watamjali. 38Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. 39Wakamkamata, wakamtupa uje ya shamba la mizabibu, wakamwua. 40Bassi atakapokuja yule bwana wa mizabibu, atawatendea nini wale wakulima? 41Wakamwambia, Atawaangamiza wabaya wale; nae atawapangisha mizabibu wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. 42Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,
Jiwe walilolikataa waashi,
Hili lilikuwa jiwe kuu la pembeni;
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu?
43Kwa sababu hii nawaambieni, ya kwamba ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na watapewa taifa lingine wenye kuzaa matunda yake. 44Nae aangukiae juu ya jiwe hili atavunjikavunjika: nae amhae litamwangukia, litampondaponda. 45Makuhani wakuu na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, wakatambua ya kuwa anawanena wao. 46Nao walipotafuta kumkamata, wakawaogopa makutano, kwa maana walimwona kuwa nabii.
Currently Selected:
Mattayo MT. 21: SWZZB1921
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: