Mattayo MT. 24
24
1YESU akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea illi kumwonyesha majengo ya hekalu. 2Yesu akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitahomolewa.
3Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakinena, Tuambie, haya yatakuwa lini? Na nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? 4Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganyeni. 5Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ni Kristo; na watadanganya wengi. 6Na mtasikia khabari za vita na uvumi wa vita: angalieni, msitishwe: maana haya hayana buddi kuwa; lakini mwisho wenyewe hado. 7Maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwako na njaa, na maradhi, na matetemeko ya inchi pahali pahali. 8Haya yote ni mwanzo wa utungu. 9Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu. 10Ndipo wengi watajikwaa, na watasalitiana, na kuchukiana. 11Na manabii wengi wa uwongo wataondoka, watadanganya wengi. 12Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, pendo la watu wengi litapoa. 13Lakini astahimiliye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka. 14Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.
15Bassi mlionapo chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama mahali patakatifu (asomae afahamu), 16ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani; 17nae aliye juu ya nyumba asishuke avichukue vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18nae aliye mashamba asirudi nyuma azichukue nguo zake. 19Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku zile! 20Ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21Maana wakati ule itakuwapo shidda kubwa, jinsi isivyopata kuwa tangu mwanzo wa ulimweugu hatta leo, wala haitakuwa kamwe. 22Na kama siku zile zisingalikatizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitakatizwa siku zile. 23Wakati huo mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko huko, msisadiki. 24Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule. 25Angalieni, nimetangulia kuwaambieni. 26Bassi wakiwaamhieni, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. 27Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 28Maana po potemzoga utakapokuwapo, ndipo tai watakapokusanyika.
29Marra baada ya shidda ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbingu zitatikisika: 30ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi. 31Nae atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya panda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande mmoja wa mwisho wa mbinguni mpaka upande wa pili.
32Kwa mtini jifunzeni mfano: tawi lake likiisha kuwa laini na kuchanua majani, mwafahamu ya kuwa wakati wa hari ni karibu; 33vivyo hivyo na ninyi, myaonapo haya yote, fahamuni ya kuwa yu karibu, tena milangoni. 34Amin, nawaambieni, Hakitapita kizazi hiki, hatta yatakapokuwa haya yote. 35Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe. 36Na khabari ya siku ile na saa ile hakuna ajuae, hatta malaika walio mbinguni, illa, Baba yangu peke yake. 37Lakini kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38Kwa maana kama vile siku ziie zilizokuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila, wakinywa, wakioa, wakioza, hatta siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39wasitambue, hatta gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 40Wakati huo watu wawili watakuwa mashamba; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; 41wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. 42Kesheni bassi: kwa maana hamwijui saa atakayokuja Bwana wenu. 43Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angalijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. 44Kwa sababu hii na ninyi mwe tayari; kwa sababu saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. 45Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake? 46Yu kheri mtumishi yule, ambae bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivi. 47Amin, nawaambieni, atamweka juu ya mali zake zote. 48Bali mtumishi yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49nae akianza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi: 50bwana wa mtumishi yule atakuja siku asiyotazamia, na saa asiyotambua, 51atamkata vipande viwili, ataweka sehemu yake pamoja na wanafiki: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.
Currently Selected:
Mattayo MT. 24: SWZZB1921
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: