YouVersion Logo
Search Icon

Marko MT. 3

3
1AKAINGIA tena katika sunagogi: na palikuwako huko mtu mwenye mkono umepooza: 2wakamvizia kuona kwamba atampotiya siku ya sabato: wapate kumshitaki. 3Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. 4Akawaambia, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua? Wakanyamaza. 5Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili: 6marra wakaloka wale Mafarisayo, wakamfanyia shauri pamoja na Maherodiano jinsi ya kumwangamiza.
7Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Watu wengi sana wakamfuata toka Galilaya, na toka Yahudi, na toka Yerusalemi, 8na toka Idumaya, na ngʼambu ya Yardani, na pande za Turo na Sidon, mkutano mkuu, waliposikia khabari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda; wakamwendea. 9Akawaambia wanafunzi wake ya kama chombo kidogo kikae karibu nae, kwa sababu ya makutano, wasije wakamsonga. 10Maana aliponya wengi, hatta wote waliokuwa na misiba wakamrukia wapate kumgusa. 11Na pepo wachafu, killa walipomwona, wahanguka mbele yake, wakalia wakinena, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu. 12Akawagombeza sana, wasimdhihirishe.
13Akapanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea. 14Akaweka thenashara, wapate kuwa pamoja nae, na kusudi awatume kukhubiri, 15na wawe na mamlaka ya kufukuza pepo. 16Na Simon akampa jina, Petro; 17na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, akawapa jina, Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo, 18na Andrea, na Filipo, na Bartolomayo, na Mattayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thaddayo na Simon Mkanani, 19na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.
20Kiisha wakaingia nyumbani; makutano wakakusanyika tena, wao wenyewe wasiweze kula hatta mkate. 21Jamaa zake walipopata khabari wakatoka kwenda kumkamata: maana walinena, Amerukwa na akili. 22Waandishi walioshuka kutoka Yahudi wakanena, Ana Beelzebul, na kwa uwezo wa mkuu wa pepo awafukuza pepo. 23Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumfukuza Shetani? 24Na ufalme nkilitinika juu ya nafsi yake ufalme ule hauwezi kusimama; 25na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba ile haiwezi kusimama. 26Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake akafitinika, hawezi kusimama, bali ana kikomo. 27Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake. 28Amin, nawaambieni, Dbambi zote watasamehewa wana Adamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; 29bali mtu atakaemkufuru Roho Mtakatifu hana masamaha hatta milele; bali atakuwa ana dhambi ya milele; 30kwa vile walivyonena, Ana pepo mchafu.
31Wakaja mama yake na ndugu zake; wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita. 32Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka; wakamwambia, Mama yako, na ndugu zako wako nje, wanakutafuta. 33Akawajibu, akinena, Mama yangu na ndugu zangu ni nani? 34Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akanena, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu. 35Kwa maana mtu ye yote atakaeyafanya mapenzi ya Mungu, huyu ndive ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

Currently Selected:

Marko MT. 3: SWZZB1921

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in