YouVersion Logo
Search Icon

Marko MT. 6

6
1AKATOKA huko, akafika hatta inchi ya kwao: wanafunzi wake wakamfuata. 2Ilipokuwa sabato, akaanza kufundisha katika sunagogi: wengi wakisikia, wakashangaa, akinena, Huyu amepata wapi haya? Na, Hekima gani hii aliyopewa huyu, na nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? 3Huyu si yule sermala, mwana wa Mariamu, na ndugu wii Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simon? na ndugu zake wanawake hawapo hapa petu? Wakachukizwa nae. 4Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, illa katika inchi yake, na kwa jamaa zake, na katika nyumba yake. 5Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. 6Akastaajahu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.
7Akawaita wale thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili; akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu: 8akawaagiza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa gongo tu, wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni: 9lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili. 10Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hatta mtakapotoka mahali pale. 11Na watu wote wasiokaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakungʼuteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu kuwa ushuhuda kwao. 12Wakatoka, wakakhubiri kwamba watu watubu. 13Wakafukuza pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagoujwa, wakawaponya.
14Mfalme Herode akasikia khabari; kwa maana jina lake limepata kutangaa, akanena, Yohana Mbatizaji amefufuka, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake. Wengine walinena, Yu Eliya. 15Wengine walinena, Huyu ni nabii au kama mmoja wa manabii. 16Lakini Herode aliposikia, alinena, Huyu ndiye Yohana, niliyemkata kichwa; amefufuka.
17Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma wata, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili va Herodias, nikewe Filipo ndugu yake: kwa kuwa amemwoa; bassi Yohana alimwambia Herode, 18Si halali kwako kuwa na mke wa ndugu yako. 19Bassi yule Herodias akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate. 20Maana Herode alimwogopa Yohana: hatta akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamhami, na alipokwisha kumsikiliza alifanya mambo mengi: nae alikuwa akimsikiliza kwa furaha. 21Hatta ilipotokea siku ya kufaa, na Herode (siku kuu ya kuzaliwa kwake) alipowafanyia karamu masheki na majemadari na watu wakubwa wa Galilaya, 22ndipo binti yake yule Herodias akaingia, akacheza, akampendeza Herode nao walioketi pamoja nae karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa. 23Akamwambia, Lo lote utakaloniomba, nitakupa hatta nussu ya ufalme wangu. 24Akatoka, akamwambia mama yake, Niombe nini? Akasema, Kichwa cha Yohana Mbatizaji. 25Marra akaingia kwa haraka mbele ya mfalme akaomba akinena, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. 26Mfalme akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya nyapo zake, na kwa ajili yao walioketi karamuni, hakutaka kumkataa. 27Marra mfalme akatuma askari, akiamuru kuleta kichwa chake. 28Akaenenda, akamkata kichwa mle gerezani, akaleta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, yule kijana akampa mama yake. 29Wauafunzi wake waliposikia khabari, wakaenda, wakachukua mayiti yake, wakamzika.
30Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa khabari za mambo yote waliyoyafanya na mambo yote waliyoyafundisha. 31Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipo watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hatta haikuwapo nafasi ya kula. 32Wakaenda zao chomboni, mahali pasipo watu, kwa faragha. 33Watu wakawaona wakienda zao, wengi wakamtambua, wakaenda huko mbio, toka miji yote, wakatanguha kufika, wakakusanyika mbele yake. 34Yesu aliposhuka chomboni, akaona makutano mengi, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kana kondoo wasio mchunga; akaanza kuwafundisha mengi. 35Hatta zikapita saa nyingi za mchana, ikawa karibu na magharibi, wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Mahali hapa nyika tupu, na sasa kunakuchwa; 36uwaage watu hawa, illi waende zao mashambani na vijijini huko na huko, wakajinunulie chakula. 37Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula: Wakamwambia, Je! twende zetu tukanunue mikate ya dinari miateen tukawape kula? 38Akawaambia, Mikale mingapi mnayo? Enendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakanena, Mitano, na samaki mbili. 39Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabiehi. 40Wakaketi kwa safu, nyingine mia, nyingine khamsimi. 41Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama mbinguni, akavibariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake awaandikie: na zile samaki mbili akawagawia wote. 42Wakala wote wakashiba. 43Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu thenashara: navyo vipande vya samaki. 44Na wanaume walioila ile mikate wapata elfu tano. 45Marra akawashurutisha wanafunzi wake wapande chomboni, watangulie kwenda ngʼambu hatta Betsaida wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano. 46Hatta alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kusali. 47Ilipokuwa jioni chombo kilikuwa kati ya bahari, na yeye peke yake katika inchi kavu. 48Akawaona wakitaahika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hatta yapata zamu ya nne ya usiku akawaendea akitemhea juu ya bahari; akataka kuwdpita. 49Nao walipomwoua anatembea juu ya bahari walidhani ya kuwa ni kivuli, wakapiga yowe, kwa sababu wote walimwona, wakafadhaika. 50Marra akasema nao, akawaambia, Jipeni moyo: ni mimi msiogope. 51Akapanda mle cbomboni walimo; npepo ukakoma; wakashangaa sana, kupita kiasi, wakastaajabu; 52kwa maana hawakufahamu khabari za ile mikate, walakini mioyo yao ilikuwa migumu.
53Hatta walipokwisha kuvuka wakafika inchi ya Genesareti, wakatia nanga. 54Na wakiisha kutoka chomboni, marra watu walimtambua, wakaenda mbio, wakizunguka inchi ile yote, 55wakaanza kuwachukua walio hawawezi vitandani, kwenda killa mahali waliposikia kwamba yupo. 56Na killa alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse walao upindo wa vazi lake: nao wote waliomgusa wakapona.

Currently Selected:

Marko MT. 6: SWZZB1921

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in