Matendo Utangulizi
Utangulizi
Kitabu cha Matendo ya Mitume ni kuendelea kwa Injili ya Luka ambapo Luka anakusudia kuonyesha kwamba yale Al-Masihi alianzisha duniani, anaendelea kuyafanya kupitia waumini wake. Kitabu hiki kinaanza na mitume wakijazwa na nguvu za Mwenyezi Mungu na kuhubiri kwa uwezo mkuu, watu 3,000 wakiokolewa katika siku moja (2:41). Maisha ya waumini wa Isa huko Yerusalemu, kuenea kwa Injili kule Samaria, huduma ya Mtume Petro, na mateso ya awali ya waumini yanafuata.
Baadaye mtazamo unamgeukia Mtume Paulo na kazi yake ya umisheni katika maeneo ya watu wa Mataifa. Safari zake tatu za umisheni zimeelezewa kwa mapana, ikimalizia na safari ya Paulo kwenda Rumi ambapo kitabu hiki kinafikia mwisho. Wasomi wengine wanapendekeza kwamba Luka alitarajia kuandika kitabu cha tatu ambacho kingeelezea kuachiliwa kwa Paulo, safari zaidi alizofanya, kushikwa na kufa kwake.
Wazo Kuu
Kitabu cha Matendo ya Mitume kiliandikwa kuonyesha kuenea kwa Injili kutoka kwa Wayahudi hadi katika maeneo ya Watu wa Mataifa (1:8). Habari njema kwamba Yesu alikufa na kufufuka tena haingeweza kufungiwa katika eneo moja la ulimwengu, lakini ilikusidiwa na Mwenyezi Mungu iwafikie watu wote. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu aliwatia nguvu watu wake ili waweze kutimiza majukumu yao. Roho wa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye nguvu hizo za kuwezesha. Uwezo mkuu wa Mwenyezi Mungu unajionyesha katika ushindi wa Injili juu ya upagani na mateso, japo huenda itagharimu wengi maisha yao (hata Petro na Paulo, ambao maisha yao yanaelezewa katika Matendo ya Mitume). Mwishowe kabisa, ushindi ni hakika kupitia Isa, aliye Bwana wetu.
Mwandishi
Luka.
Mahali
Hapajulikani.
Tarehe
Kama 60–70 BK.
Mgawanyo
Siku za mwanzo za waumini wa Isa Al-Masihi (1:1–5:42)
Mateso na kupanuka (6:1–9:31)
Huduma ya kueneza Injili ya Petro (9:32–12:25)
Safari ya kwanza ya Paulo kueneza Injili (13:1–14:28)
Mkutano wa Yerusalemu (15:1-41)
Safari ya pili ya Paulo kueneza Injili (16:1–18:22)
Safari ya tatu ya Paulo kueneza Injili (18:23–21:14)
Kukamatwa kwa Paulo, na safari yake kwenda Rumi (21:15–28:31).
Currently Selected:
Matendo Utangulizi: NMM
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018 by Biblica, Inc.
Used with permission.
All rights reserved worldwide.

: