Yohana 11:43-44
Yohana 11:43-44 NEN
Baada ya kusema haya, Yesu akapaza sauti yake akaita, “Lazaro, njoo huku!” Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.”