YouVersion Logo
Search Icon

Ezekieli 19

19
Maombolezo
1Mungu aliniambia niimbe utenzi huu wa maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli:
2Mama yenu alikuwa simba wa fahari
miongoni mwa simba wengine.
Alikaa kati ya simba vijana,
akawalisha watoto wake.
3Alimlea mtoto mmojawapo wa watoto wake,
mtoto huyo naye akawa simba kijana hodari.
Akajifunza kwa mama yake kuwinda,
akawa simba mla watu.
4Mataifa yakapiga mbiu ya hatari dhidi yake,
wakamnasa katika mtego wao,
wakampeleka kwa ndoana mpaka Misri.
5Mama yake alipoona kuwa amechoka kungoja,
matumaini ya kumpata yamekwisha,
alimchukua mtoto wake mwingine,
akamfanya simba kijana hodari.
6Huyo alipokuwa amekua,
akaanza kuzurura na simba wengine.
Naye pia akajifunza kuwinda,
akawa simba mla watu.
7Aliziandama ngome za watu
na kuiharibu miji yao.
Nchi ikatishika pamoja na wakazi wake,
kwa sauti ya kunguruma kwake.
8Mataifa yakamkabili kutoka mkoani mwao kote,
wakatandaza wavu wao juu yake,
naye akanaswa katika mtego wao.
9Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao,
wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni.
Huko, wakamtia gerezani,
ili ngurumo yake isisikike tena
juu ya milima ya Israeli.
10Mama yako alikuwa kama mzabibu shambani,
uliopandikizwa kando ya maji,
ambao ulizaa sana kwa kuwa na maji tele.
11Ulikuwa na matawi yenye nguvu,
ambayo yalikuwa fimbo za kifalme.
Mzabibu huo ulikua kupita miti mingine,
watu waliusifu ukubwa wa shina lake
na wingi wa matawi yake.
12Lakini ulingolewa kwa hasira
ukatupwa chini ardhini;
upepo wa mashariki ukaukausha,
matunda yake yakapukutika;
matawi yake yenye nguvu yalikaushwa,
nao moto ukauteketeza.
13Na sasa umepandikizwa jangwani,
katika nchi kame isiyo na maji.
14Lakini moto umetoka kwenye shina lake,
umeyateketeza matawi na matunda yake.
Matawi yake kamwe hayatakuwa na nguvu,
wala hayatakuwa fimbo za kifalme.
Huo umekuwa wimbo wa maombolezo; ndivyo unavyoimbwa daima.

Currently Selected:

Ezekieli 19: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in