YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 6

6
Mungu amwita Isaya kuwa nabii
1 #6:1 Taz 2Fal 15:7 2Nya 26:23 Mnamo mwaka aliofariki mfalme Uzia, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi kilicho juu na cha fahari. Pindo la vazi lake lilienea hekaluni mote, 2na juu yake walikuwa wamekaa malaika.#6:2 malaika: Au Maserafi. Kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Mawili ya kufunika uso, mawili ya kufunika mwili na mawili ya kurukia. 3#6:3 Taz Ufu 4:8 Waliitana kila mmoja na mwenzake hivi:
“Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu,
ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi!
Dunia yote imejaa utukufu wake.”
4 #6:4 Taz Ufu 15:8 Sauti yao iliitikisa misingi ya milango ya hekalu, nalo likajaa moshi.
5Basi, mimi nikasema, “Ole wangu! Mimi nimeangamia, maana, midomo yangu ni najisi, na watu ninaoishi nao ni najisi kama mimi. Hata hivyo, kwa macho yangu mwenyewe, nimemwona Mfalme, Mwenyezi-Mungu wa majeshi.”
6Basi, mmoja wa hao malaika akaruka kunijia, akiwa ameshika mkononi koleo lililokuwa na kaa la moto alilolitwaa madhabahuni. 7Naye akinigusa nalo mdomoni, akasema: “Tazama, kaa hili limekugusa mdomo; umeondolewa hatia yako, umesamehewa dhambi yako.”
8Kisha nikamsikia Mwenyezi-Mungu akisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekuwa mjumbe wetu?” Nami nikajibu, “Niko hapa! Nitume mimi.”
9Naye akaniambia, “Nenda ukawaambie watu hawa:
‘Mtasikiliza sana, lakini hamtaelewa;
mtatazama sana, lakini hamtaona.’”
10Kisha akaniambia,
“Zipumbaze akili za watu hawa,
masikio yao yasisikie,
macho yao yasione;
ili wasije wakaona kwa macho yao,
wakasikia kwa masikio yao,
wakaelewa kwa akili zao,
na kunigeukia, nao wakaponywa.”
11Mimi nikauliza,
“Bwana, mpaka lini?”
Naye akanijibu,
“Mpaka hapo miji itakapobaki tupu bila wakazi,
nyumba bila watu,
na nchi itakapoharibiwa kabisa.
12Nami Mwenyezi-Mungu nitawapeleka watu mbali,
na kuifanya nchi yote kuwa mahame.
13Hata wakibaki watu asilimia kumi,
nao pia watateketezwa.
Hao watakuwa kama mvinje au mwaloni
ambao kisiki chake kimebaki baada ya kukatwa.”
(Kisiki hicho ni mbegu takatifu ya chanzo kipya.)

Currently Selected:

Isaya 6: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in