YouVersion Logo
Search Icon

Yobu 9

9
Jibu la Yobu
1Kisha Yobu akajibu:
2 # Taz Yobu 4:17 “Kweli najua hivyo ndivyo ilivyo.
Lakini mtu awezaje kuwa mwema mbele ya Mungu?
3Kama mtu angethubutu kushindana naye,
hataweza kufika mbali;
hata kujibu swali moja kati ya elfu.
4Yeye ni mwenye hekima mno na nguvu nyingi,
nani aliyepingana naye, akashinda?
5Yeye huiondoa milima bila yenyewe kutambua,
huibomolea mbali kwa hasira yake.
6Yeye huitikisa dunia kutoka mahali pake,
na nguzo zake zikatetemeka.
7 # Taz Bar 2:34-35 Huliamuru jua lisichomoze
huziziba nyota zisiangaze.
8Yeye peke yake alizitandaza mbingu,
na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.#9:8 na … bahari: Au alilikanyaga dude la baharini mgongoni.
9 # Taz Yobu 38:31, Amo 5:8 Ndiye aliyezifanya nyota angani:
Dubu, Orioni, Kilimia, na nyota za kusini.
10Ndiye atendaye makuu yasiyoeleweka,
mambo ya ajabu yasiyo na idadi.
11Loo! Hupita karibu nami nisimwone,
kisha huenda zake bila ya mimi kumtambua.
12Tazama! Yeye huchukua anachotaka;
nani awezaye kumzuia?
Nani awezaye kumwuliza: ‘Unafanya nini?’
13“Mungu hatazuia hasira yake;
chini yake wainama kwa hofu Rahabu#9:13 Rahabu: Taz 7:12 na maelezo yake. na wasaidizi wake.
14Nitawezaje basi kumjibu Mungu?
Nitachagua wapi maneno ya kumwambia?
15Ingawa sina hatia, siwezi kumjibu.
Lazima kumwomba anihurumie huyo mshtaki wangu.
16Hata kama ningemwita naye akajibu,
nisingeweza kuamini kuwa ananisikiliza.
17Yeye huniponda kwa dhoruba;
huongeza majeraha yangu bila sababu.
18Haniachi hata nipumue;
maisha yangu huyajaza uchungu.
19Kama ni kushindana, yeye ana nguvu mno!
Na kama ni kutafuta juu ya haki,
nani atakayemleta#9:19 atakayemleta: Makala ya Kiebrania: Atanileta. mahakamani?
20Ingawa sina hatia, maneno yangu yenyewe yangenihukumu;
ingawa sina lawama, angenithibitisha kuwa mpotovu.
21Sina lawama, lakini sijithamini.
Nayachukia maisha yangu.
22Yote ni mamoja, kwa hiyo nasema;
Mungu huwaangamiza wema na waovu.
23Maafa yaletapo kifo cha ghafla,
huchekelea balaa la wasio na hatia.
24Nchi ikitiwa watu waovu katika utawala wa mwovu,
Mungu huyafumba macho ya mahakimu wake!
Kama si yeye afanyaye hivyo, ni nani basi?
25“Siku zangu zaenda mbio kuliko mpiga mbio;
zinakimbia bila kuona faida.
26Zapita kasi kama mashua ya matete;
kama tai anayerukia mawindo yake.
27Nasema: ‘Nitasahau lalamiko langu,
niondoe uso wangu wa huzuni na kuwa na furaha!’
28Lakini nayaogopa maumivu yangu yote,
kwani najua Mungu hataniona kuwa sina hatia.
29Ikiwa nitahukumiwa kuwa na hatia,
ya nini basi nijisumbue bure?
30Hata kama nikitawadha kwa theluji,
na kujitakasa mikono kwa sabuni,
31hata hivyo, atanitumbukiza shimoni kwenye uchafu,
na mavazi yangu yataniona kuwa kinyaa.
32Mungu si mtu kama mimi niweze kumjibu,
hata tuweze kwenda mahakamani pamoja.
33Hakuna msuluhishi kati yetu,
ambaye angeamua kati yetu sisi wawili.
34Mungu na aniondolee hiyo fimbo ya kunipiga,
na kitisho chake kisinitie hofu!
35Hapo ningeweza kusema bila kumwogopa;
kwani sivyo nilivyo nafsini mwangu.#9:35 kwani … mwangu: Tafsiri ngumu. Tafsiri nyingine: Lakini kwangu … sivyo ilivyo.

Currently Selected:

Yobu 9: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in