YouVersion Logo
Search Icon

Hesabu UTANGULIZI

UTANGULIZI
Jina la kitabu hiki, “Hesabu” latokana na Kigiriki “Arithmoi” na Kilatini “Numeri”. Kuna orodha mbalimbali za watu na hesabu au sensa mbili za Waisraeli ambazo zinatajwa katika kitabu chenyewe. Katika kitabu hiki (cha nne miongoni mwa vitabu vitano vya kwanza vya Biblia), tunaelezwa jinsi Mose alivyowahesabu Waisraeli kabla ya kuanza safari yao kutoka mlima Sinai, na tena baadaye katika nchi ya Moabu, mashariki ya mto Yordani. Kitabu hiki cha Hesabu chakamilisha na kumaliza masimulizi ya vitabu vya Kutoka na Walawi.
Kitabu chenyewe chaeleza jinsi Waisraeli baada ya kupokea maagizo yote ya Mungu kule Sinai, walisafiri jangwani kuelekea nchi ya ahadi (1:1–10:10). Kwanza waliwasili Kadeshi Barnea kusini mwa nchi hiyo, lakini hawakufaulu kuingia. Hivyo ikawabidi kukaa jangwani miaka arubaini, muda ambapo walijitayarisha na mwishowe wakaichukua nchi ya Moabu mashariki mwa Bahari ya Chumvi (10:11–21:35). Sura za mwisho za kitabu hiki zinasimulia matukio yaliyohusu kutekwa kwa nchi ya Moabu; kutoka humo Waisraeli wataingia katika nchi waliyoahidiwa (22:1–36:13).
Kitabu hiki kinatupa picha ya Waisraeli katika hali yao halisi ya kibinadamu wenye matumaini na mashaka, wenye nguvu na dhaifu. Kinaonesha pia uaminifu wa Mungu katika kuwalinda watu wake.

Currently Selected:

Hesabu UTANGULIZI: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in