Methali 6
6
Maonyo manne
1Mwanangu, kama umejitolea kumdhamini jirani yako,
ikiwa umetoa ahadi yako kwa ajili ya mtu huyo,
2umejibana kwa maneno yako mwenyewe,
umejinasa kwa ahadi uliyofanya.
3Ujue kwamba uko chini ya mamlaka ya mwenzio,
lakini mwanangu, ukitaka kujiokoa, basi fanya hivi:
Mwendee mtu huyo mara moja umsihi akupe uhuru wako.
4Jitahidi usiache macho yako yapate usingizi,
wala kope za macho yako zisinzie.
5Jiokoe kwa kujitoa katika mtego huo,
mithili ya paa ama ndege amtorokavyo mwindaji.
6Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi,
fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima.
7Sisimizi hana kiongozi, ofisa, wala mtawala;
8lakini hujiwekea chakula wakati wa kiangazi,
hujikusanyia akiba wakati wa mavuno.
9Ewe mvivu, utalala hapo mpaka lini?
Utaamka lini katika usingizi wako?
10Wasema: “Acha nilale kidogo tu,
acha nisinzie kidogo!
Niache nikunje mikono nipumzike kidogo!”
11Wakati huo umaskini utakuvamia kama mnyanganyi,
ufukara utakufuata kama jambazi.#6:11 Taz pia 24:33-34
12Mtu mwovu, mtu asiyefaa kitu,
huzururazurura akisema maneno mapotovu.
13Hukonyeza jicho kuwakosesha wengine,
huparuza kwa nyayo,
na kuashiria watu kwa vidole.
14Akiwa amejaa ulaghai moyoni hutunga maovu,
huzusha ugomvi kila mahali.
15Kutokana na hayo maafa yatamvamia ghafla,
ghafla atadhurika vibaya asiweze kupona tena.
16Kuna vitu sita anavyochukia Mwenyezi-Mungu;
naam, vitu saba ambavyo ni chukizo kwake:
17Macho ya kiburi,
ulimi mdanganyifu,
mikono inayoua wasio na hatia,
18moyo unaopanga mipango miovu,
miguu iliyo mbioni kutenda maovu,
19shahidi wa uongo abubujikaye uongo,
na mtu achocheaye fitina kati ya ndugu.
Onyo dhidi ya uasherati
20Mwanangu, shika maagizo ya baba yako,
wala usisahau mafundisho ya mama yako;
21yaweke daima moyoni mwako,
yafunge shingoni mwako.
22Yatakuongoza njiani mwako,
yatakulinda wakati ulalapo,
yatakushauri uwapo macho mchana.
23Maana amri hiyo ni taa,
na sheria hiyo ni mwanga.
Maonyo hayo na nidhamu yatuweka njiani mwa uhai.
24Yatakulinda mbali na mwanamke mbaya,
yatakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni.#6:24 Taz 5:5 maelezo.
25Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake,
wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake.
26Mtu hupoteza kipande cha mkate kwa malaya,
lakini kwa mke wa mtu mwingine utapoteza uhai wako wote.
27Je, waweza kuweka moto kifuani
na nguo zako zisiungue?
28Je, waweza kukanyaga makaa ya moto
na nyayo zako zisiungue?
29Ndivyo alivyo mwanamume alalaye na mke wa mwenzake;
yeyote anayemgusa mwanamke huyo hataacha kuadhibiwa.
30Watu hawambezi sana mtu akiiba kwa sababu ya njaa;
31lakini akipatikana lazima alipe mara saba;
tena atatoa mali yote aliyo nayo.
32Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa;
huyo hujiangamiza yeye mwenyewe.
33Atapata majeraha na madharau;
fedheha atakayopata haitamtoka.
34Maana wivu wa mume humfanya kuwa mkali kabisa;
wakati atakapolipiza kisasi hana cha kuhurumia.
35Hatakubali fidia yoyote;
wala kutulizwa na zawadi zako nyingi.
Currently Selected:
Methali 6: BHN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

: