Zaburi 106
106
Wema wa Mungu kwa watu wake
1 # Taz Zab 11:5; 107:1; 118:1; 136:1 Haleluya! Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema;
kwa maana fadhili zake zadumu milele!
2Ni nani awezaye kutaja matendo ya Mwenyezi-Mungu?
Ni nani awezaye kumsifu kama anavyostahili?
3Heri wale wanaotekeleza haki,
wanaotenda daima mambo yaliyo sawa.
4Unikumbuke ee Mwenyezi-Mungu unapowafadhili watu wako;
unisaidie wakati unapowaokoa;
5ili niweze kuona fanaka ya wateule wako,
nipate kufurahia furaha ya taifa lako,
na kuona fahari pamoja na watu wako.
6Tumetenda dhambi sisi na wazee wetu;
tumetenda maovu, tumefanya mabaya.
7Wazee wetu walipokuwa Misri,
hawakujali matendo ya ajabu ya Mungu;
hawakukumbuka wingi wa fadhili zake,
bali walimwasi kando ya bahari ya Shamu.
8Hata hivyo Mungu aliwaokoa kama alivyoahidi,
ili aoneshe nguvu yake kuu.
9Aliikemea bahari ya Shamu ikakauka;
akawapitisha humo kama katika nchi kavu.
10Aliwaokoa mikononi mwa waliowachukia;
aliwaokoa kutoka kwa nguvu za maadui zao.
11Maji ya bahari yaliwafunika maadui zao;
wala hakusalia hata mmoja wao.
12Hapo watu wake wakaamini maneno yake,
wakamwimbia tenzi za sifa yake.
13Lakini mara walisahau matendo yake,
wakaacha kutegemea shauri lake.
14Walijawa na tamaa kubwa kule jangwani,
wakamjaribu Mungu kule nyikani.
15Naye akawapa kile walichoomba,
lakini akapeleka maradhi mabaya kati yao.
16Kule kambini walimwonea wivu Mose,
na Aroni mtumishi mtakatifu wa Mwenyezi-Mungu.
17Ndipo ardhi ikafunguka ikammeza Dathani,
na kumzika Abiramu na kundi lake lote;
18moto ukawatokea wafuasi wao,
ukawateketeza watu hao waovu.
19Walitengeneza ndama wa dhahabu kule Horebu,
wakaiabudu sanamu hiyo ya kusubu;
20waliubadilisha utukufu wa Mungu,
kwa sanamu ya mnyama ambaye hula nyasi.
21Walimsahau Mungu aliyewaokoa,
aliyetenda mambo makuu nchini Misri,
22maajabu katika nchi hiyo ya Hamu,
na mambo ya kutisha katika bahari ya Shamu.
23Mungu alisema atawaangamiza watu wake,
ila tu Mose mteule wake aliingilia kati,
akaizuia hasira yake isiwaangamize.
24Kisha wakaidharau nchi ile ya kupendeza,
kwa sababu hawakuwa na imani na ahadi ya Mungu.
25Walinungunika mahemani mwao,
wala hawakumsikiliza Mwenyezi-Mungu.
26Hivyo Mungu akainua mkono akaapa
kwamba atawaangamizia jangwani;
27atawatawanya wazawa wao kati ya watu,
na kuwasambaza duniani kote.
28Kisha wakajiunga kumwabudu Baali kule Peori,
wakala tambiko zilizotambikiwa mizimu.
29Waliichochea hasira ya Mwenyezi-Mungu kwa matendo yao,
maradhi mabaya yakazuka kati yao.
30Lakini Finehasi akasimama kufanya malipizi,
na yale maradhi yakakoma.
31Jambo hilo lakumbukwa kwa heshima yake,
tangu wakati huo na nyakati zote.
32Walimkasirisha Mungu penye maji ya Meriba,
Mose akapata taabu kwa ajili yao.
33Walimtia Mose uchungu rohoni,
hata akasema maneno bila kufikiri.
34Hawakuwaua watu wa mataifa mengine
kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru.
35Bali walijumuika na watu wa mataifa,
wakajifunza kutenda mambo yao.
36Waliabudu sanamu za miungu yao,
nazo zikawa mtego wa kuwaangamiza.
37Waliwaua watoto wao wa kiume na wa kike,
wakawatoa tambiko kwa pepo.
38Walimwaga damu ya wasio na hatia,
damu ya watoto wao wa kiume na wa kike
ambao waliwatoa tambiko kwa sanamu za Kanaani,
nayo nchi ikatiwa unajisi kwa mauaji hayo.
39Hivyo wakafanywa najisi kwa matendo yao,
2wakakosa uaminifu kwa Mungu kama wazinzi.
40Hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawawakia watu wake,
akachukizwa sana na hao waliokuwa mali yake.
41Akawatia makuchani mwa watu wa mataifa,
hao wenye kuwachukia wakawatawala.
42Maadui zao waliwakandamiza,
wakawatumikisha kwa nguvu.
43Mara nyingi Mungu aliwaokoa watu wake,
lakini wao wakachagua kumwasi,
wakazidi kuzama katika uovu wao.
44Hata hivyo Mungu alizijali taabu zao,
wakati aliposikia kilio chao;
45kwa ajili yao alilikumbuka agano lake,
akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake.
46Aliwafanya waliowakandamiza wawaonee huruma.
47Utuokoe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,
utukusanye pamoja kutoka kwa mataifa,
tupate kulisifu jina lako takatifu,
na kuona fahari juu ya sifa zako.
48Asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli,
tangu milele na hata milele!
Na watu wote waseme: “Amina!”
Asifiwe Mwenyezi-Mungu!
Currently Selected:
Zaburi 106: BHN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

: