YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 141

141
Hatari za tamaa mbaya
(Zaburi ya Daudi)
1Nakuita, ee Mwenyezi-Mungu,
uje haraka kunisaidia!
Uisikilize sauti yangu wakati ninapokuita!
2 # Taz Ufu 5:8 Sala yangu uipokee kama ubani;
niinuapo mikono yangu kwako unikubali kama tambiko ya jioni.
3Ee Mwenyezi-Mungu ukilinde kinywa changu,
uweke ulinzi mlangoni mwa mdomo wangu.
4Unikinge nisielekee kufanya mabaya,
nisijishughulishe na matendo maovu;
nisijiunge na watu watendao mabaya,
wala nisishiriki kamwe karamu zao.
5Afadhali mtu mwema anipige kunionya;
lakini sikubali kamwe kusifiwa na wabaya,
maana nasali daima dhidi ya maovu yao.#141:5-7 maana katika Kiebrania si dhahiri.
6Wakuu wao watakapopondwa miambani,
ndipo watatambua maneno yangu yalikuwa sawa.
7Mifupa yao itatawanywa mdomoni pa Kuzimu
kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande!
8Bali mimi nakutegemea, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu;
ninakimbilia usalama kwako, usiniache hatarini.
9Unikinge na mitego waliyonitegea,
uniepushe na matanzi ya hao watu waovu.
10Waovu wanaswe katika mitego yao wenyewe,
wakati mimi najiendea zangu salama.

Currently Selected:

Zaburi 141: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in