YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 59

59
Sala ya kuomba ulinzi wa Mungu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo “Usiharibu”. Utenzi wa Daudi wakati Shauli alipotuma wapelelezi wamuue)
1Ee Mungu wangu, uniokoe na maadui zangu;
unikinge na hao wanaonishambulia.
2Uniokoe na hao wanaotenda maovu;
unisalimishe kutoka kwa hao wauaji!
3Tazama! Wananivizia waniue;
watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu.
4Bila ya kosa, hatia au dhambi yangu,
wanakimbia, ee Mwenyezi-Mungu, kujiweka tayari.
Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu,
ukatazame na kunisaidia!
5Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu,
Mungu Mwenye Nguvu, Mungu wa Israeli.
Uamke, uwaadhibu hao watu wasiokujua;
usiwaache hao wanaopanga ubaya.
6Kila jioni maadui hao hurudi
wakibweka kama mbwa,
na kuzungukazunguka mjini.
7Tazama, ni matusi tu yatokayo mdomoni mwao,
maneno yao yanakata kama upanga mkali;
tena wanafikiri hakuna anayewasikia.
8Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawacheka;
unawapuuza hao watu wote wasiokujua.
9Nitakungoja, ewe uliye nguvu yangu;
maana wewe, ee Mungu, u ngome yangu.
10Mungu wangu utanijia na fadhili zako,
utaniwezesha kuwaona maadui zangu wameshindwa.
11Usiwaue mara moja, watu wangu wasije wakasahau;
ila uwayumbishe kwa nguvu yako, uwaporomoshe chini.
Ee Bwana, wewe ndiwe ngao yetu!
12Wao hutenda dhambi kwa yote wasemayo,
kwa hiyo na wanaswe katika kiburi chao!
Kwa sababu ya laana na uongo wao,
13uwateketeze kwa hasira yako,
uwateketeze wasiwepo tena;
ili watu wote wajue kuwa wewe ee Mungu
watawala wazawa wa Yakobo
hata mpaka miisho ya dunia.
14Kila jioni maadui hao hurudi
wakibweka kama mbwa,
na kuzungukazunguka mjini.
15Hupitapita huko na huko wakitafuta mlo,
na wasipotoshelezwa hunguruma.
16Lakini mimi nitaimba sifa za nguvu yako;
nitashangilia asubuhi juu ya fadhili zako;
maana wewe umekuwa ngome yangu
na kimbilio langu wakati wa taabu.
17Ewe uliye nguvu yangu, nitakuimbia sifa;
ee Mungu, wewe u ngome yangu;
Mungu mwenye kunifadhili!

Currently Selected:

Zaburi 59: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in