YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 61

61
Kuomba ulinzi
(Kwa Mwimbishaji: Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi)
1Ee Mungu, usikie kilio changu,
usikilize sala yangu.
2Ninakulilia kutoka miisho ya dunia,
nikiwa nimevunjika moyo.
Uniongoze juu kwenye mwamba mkubwa#61:2 mwamba mkubwa: Kiebrania: Mwamba, neno litumikalo mara kwa mara katika mashairi kumtaja Mungu na kumfananisha na mlima ambako watu waweza kukimbilia usalama.
3maana wewe ndiwe kimbilio langu,
kinga yangu imara dhidi ya adui.
4Naomba nikae nyumbani mwako milele
nipate usalama chini ya mabawa yako.
5Ee Mungu, umezisikia ahadi zangu,
umenijalia sehemu yangu unayowapa wale wakuchao.
6Umjalie mfalme maisha marefu,
miaka yake iwe ya vizazi vingi.
7Atawale milele mbele yako, ee Mungu;
fadhili na uaminifu wako vimlinde.
8Hivyo nitakuimbia nyimbo za sifa,
nikizitekeleza ahadi zangu kila siku.

Currently Selected:

Zaburi 61: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in