Zaburi 64
64
Sala ya kuomba ulinzi wa Mungu
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)
1Usikie, ee Mungu, lalamiko langu;
yalinde maisha yangu na vitisho vya maadui.
2Unikinge na njama za waovu,
na ghasia za watu wabaya.
3Wananoa ndimi zao kama upanga,
wanafyatua maneno ya ukatili kama mishale.
4Toka mafichoni wamshambulia mtu mnyofu,
wanamshambulia ghafla bila kuogopa.
5Wanashirikiana katika nia yao mbaya;
wanapatana mahali pa kuficha mitego yao.
Wanafikiri: “Hakuna atakayeweza kuiona.”
6Hufanya njama zao na kusema:
“Sasa tumekamilisha mpango!
Nani atagundua hila zetu?”
Mipango ya siri imefichika moyoni mwa mtu!#64:6 maana ya aya ya 6 katika Kiebrania si dhahiri.
7Lakini Mungu atawapiga mishale,
na kuwajeruhi ghafla.
8Atawaangamiza kwa sababu ya maneno yao;#64:8 Atawaangamiza … yao: Au Maneno yao yatawaangamiza.
kila atakayewaona atatikisa kichwa.
9Hapo watu wote wataogopa;
watatangaza aliyotenda Mungu,
na kufikiri juu ya matendo yake.
10Waadilifu watafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu,
na kukimbilia usalama kwake;
watu wote wanyofu wataona fahari.
Currently Selected:
Zaburi 64: BHN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

: